Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Jana nilikuwa kwenye ile page ya Tume Huru ya Uchaguzi.
Mpaka sasa hii tume imeshapita Zanzibar, Arusha, Pwani, Songwe, Ruvuma na Rukwa na kuanzia Machi 1 wataanza kuandikisha wapiga kura huko Mkoani Morogoro.
Kwa namna ambavyo nawaona Gen Z (watu waliozaliwa 1997 - 2012) yaani ni kama hawajui kinachoendelea kabisa.
Wengi wao ukiwafuata kuwauliza, hawana hata habari kwamba kuna mchakato unaoendelea wa kujiandikisha na kuboresha taarifa zako kwenye daftari la mpiga kura
Hii process ni kama wamejitenga nayo. Focus ipo kwa harusi ya Aziz Ki na Hamisa, Ali Kamwe kumjengea nyumba mama yake na penzi la Diamond na yule dada wa kuitwa Rita.
Soma pia: Fatma Karume atamani Watanzania Wangekuwa na Ufahamu kama Gen Z wa Kenya
Yaani a typical Tanzanian Gen Z hajui, haelewi na hana taarifa zozote kuhusu mchakato wa kuboresha taarifa zake ili aweze kupiga kura mwezi Oktoba
Hata ukiangalia picha ambazo zinapostiwa kwenye Instagram ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, wengi wanaojiandikisha ni wazee na watu wazima.
Bora hata zamani kulikuwa na ufuatiliaji kidogo kwa sababu, kile kitambulisho cha mpiga kura kilikuwa kinatumika kwenye matumizi mengine pia kama kufungua akaunti za benki n.k lakini sasa hivi mtu anaona namba ya NIDA anayo, yaani hajisumbui kabisa kufuatilia kuhusu kitambulisho.
Ushauri kwa tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Kama kweli mnataka Gen Z wajiandikishe acheni kutumia TBC na Channel Ten kutangaza shughuli zenu. Anzeni kupeleka matangazo yenu pale Bongo Trending, Simulizi na Sauti, Rick Media na media nyingine ambazo zinafuatiliwa na vijana.