Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Swali dogo ukiambiwa uoe mke usiyemjua utakubali?Nimekuwa nawaza;
Kutokana na utaratibu Tanzania waliojiwekea kwa EWURA kutoa Bei Elekezi ya kuuzia mafuta (petrol), kwa nini TRA wasitumie hiyo fursa kwa kukusanya kodi ya mafuta kule Bandarani wakati yakitoka na kuepuka gharama za ukusanyaji kodi pamoja na usumbufu kwa wamilikaji wa vituo.
Namaanisha; TRA waweke kodi yao kabisa ndio mafuta yatoke bandarini
Faida za huu utaratibu niliopendekeza
1. Kuondoa kabisa gharama za ununuzi wa mashine za Receipts na matengenezo yake.
2. Kuondoa kabisa tatizo la ukwepaji kodi.
3. Kuondoa task force inayohusika kuzunguka vituo vya mafuta kufuatilia receipts/kodi.
4. Kupunguza kabisa gharama za kukusanya kodi ya mafuta pengine kwa 75%.
5. Kuokoa fedha nyingi kwa mamilioni ambayo hutumika wakati wa kukusanya kodi hiyo.
Kwa sasa ukipita vituo vya mafuta utakupa makapu yamejaa receipts, naona kama nikuongeza gharama?
Naomba mtu aniwekee hasara za kutumia huu mfumo niliopendekeza. Sitamani kusikia reference sijui kutoka kwa professor gani wa account kwani lengo la mada yangu ni kufanya watu wafikiri kama kuna njia bora na rafiki zaidi kwa mazingira yetu na sio lazima kufuata mfumo wa wale waliotutawala (copy paste)
Nitoe angalizo kuwa, mimi sio mbobezi wa masomo ya account hivyo natamani kujua zaidi.
Duh kiongozi umetoa elimu kwa mlipa kodi watu wote kimyaSwali dogo ukiambiwa uoe mke usiyemjua utakubali?
Kodi haitozwi hivo kama unavyofikiria , kodi ni mahesabu kuna kuangalia mauzo ,garama za biashara, manunuzi n.k. Sasa unataka mtu kaleta tani 200n za mafuta alipe kodi je akishindwa uza yote, je garama zake za biashara zikibadilika badilika, je akiuza kwa bei ya juu zaidi. Ndiyo maana kodi inatozwa kwa kuangalia mambo hayo makuu 3 manunuzi,garama na mauzo.Huwezi toza kodi mtuu kwenye kitu hajauza bado.EFD tra wao wameleta kama nyenzo ya kuwasaidia kujua mauzo na pia mtumiaji yaani mmiliki wa efd kama nyenzo yake ya kutunza kumbukumbu.ili pande zote mbili tra na muuzaji kuweza weka mazingira ya kujua kiasi cha kutoza nyenzo hiyo ndiyo huwezesha taarifa muhimu ya mauzo.