Hivi hakuna teknolojia nzuri ya kurudishia "mabampa" ya magari?

Hivi hakuna teknolojia nzuri ya kurudishia "mabampa" ya magari?

ERoni

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2013
Posts
48,052
Reaction score
104,677
Wakuu,

Naomba kujua toka kwa mafundi na wenye uzoefu, hivi hakuna teknolojia nzuri ya kurudishia mabampa ya hizi gari? Maana naona gari nyingi sasa hivi tena "mpya kutoka Japan" zinang'oka sana mabampa yake.

Nimekutana na Lexus RX300 ina misumari ya gypsum boards balaa, yaani hadi uzuri wa gari umepotea kabisa. Gari ni DN.. lakini imejaa screw za gypsum. Sio hilo tu, zipo IST, Noah, Ipsum, Isis nk nyingi tu zipo ovyo sana mabampa yake.

Wataalamu tiririkeni hapa, kwamba mmeshindwa au ni ubahili wa wenye vyombo vyao.
 
Tatizo watu wanapeleka magari yao kwa mafundi uchwara peleka gari yako kwa mchina au garage yoyote nzuri uone kama watakufungia hayo ma screw.
 
Watu wanapenda sana cheap service,mtu anamiliki gari ya million 20 ikipata shida ya kunyosha/kurudishia bumper anapeleka kwa fundi makarai hapo unategemea nini?
 
Hiyo shida iko kwenye gari za Japan tu,chunguza halafu leta mrejesho...
 
Tatizo watu wanapeleka magari yao kwa mafundi uchwara peleka gari yako kwa mchina au garage yoyote nzuri uone kama watakufungia hayo ma screw.
Well, hapo sawa. Kwa garage za viwango wanatengeneza kwa standard zinazotakiwa.

Hivi mtu anamiliki gari ya 30mil, anashindwaje kufanya maintenance ya 'bumper' hadi kulifunga screw za gypsum board?
 
Kinacho washinda watu wengi ni maintenance mkuu mtu kutoa ml 30 haoni uchungu lkn mwambie kutengeneza gari ni laki tano uone povu lake, kuna boss wangu mmoja anakuambia ukitaka kujua mtu anapesa angalia gari analotembelea lipo katika muonekano gani hata kama ni ist huwezi kuta ina mikwaruzo coz akipata anapeleka kurekebisha kina sisi unakuta gari inaramani za kutosha utazani umepaka rangi ya nyumba
Well, hapo sawa. Kwa garage za viwango wanatengeneza kwa standard zinazotakiwa.

Hivi mtu anamiliki gari ya 30mil, anashindwaje kufanya maintenance ya 'bumper' hadi kulifunga screw za gypsum board?
 
Back
Top Bottom