sangujoseph
Senior Member
- Nov 30, 2015
- 164
- 183
By Sangu Joseph
Kwa mara nyingine tena naomba nimzungumzie Bwana Konde Boy (Harmonize), lengo la kuchambua hili ni kuchagiza tu kwenye game ya BongoFleva, si kumkosoa mtu yeyote Ila tunamchambua ili asomapo mwenyewe ajue kuna watu wanaliona jambo lake kwa upande wa pili.
Toleo lililopita nilieleza namna ambavyo Harmonize atamuacha Alikiba kutokana na kuwa na project za mara kwa mara, kama ulikosa soma hapa (Namuona Alikiba akiachwa na Harmonize - JamiiForums)
Leo nataka nizungumzie kuhusiana na uamuzi wake Konde Boy wa kumtambulisha Msanii wa kwanza wa Konde Gang Ibraa TZ sitaki kuzungumzia uwezo wa Ibraah bali nitausema baadaye, Ila kiufupi kwa sasa anapaswa kuungwa mkono, kwa sababu ni mfanyakazi mpya kwenye kiwanda cha BongoFleva.
Tuje hapa Harmonize kwa sasa nadhani, amewahi sana kumtambulisha msanii wake, kwa sababu hata yeye mwenyewe bado alikua kwenye Process ya kujitangaza mtaani.
Harmonize alikua katika kipindi cha kujitambulisha mtaani, na kujenga empire yake Konde Gang, tangu alivyotoka kwenye Label yake ya zamani WCB Wasafi , ndiyo maana tuliona alikua akifanya matamasha mengi sana kwa muda mfupi, na uzinduzi wa kibabe wa album.
Hii hatua ya kuanza kumsimamisha Ibraah TZ nadhani itamuwia ugumu kidogo, kwa sababu bado hata yeye mwenyewe Mtaa hajaumasta vizuri kama kafikia Asilimia 80 tu.
Mimi kama ningebahatika kukutana naye ningemshauri angesubiri kidogo, mpaka project ya Album yake #Afroeast iishe ndiyo angeanza kusimamia Msanii, kwanini nasema hivyo, kwa sababu kuna wakati ilimbidi DiamondPlatnumz kujipa likizo ya muda mrefu ili wasanii wake wasimame, na aliweza kufanya hivyo kwa sababu tayari alishaunyaka kitaa cha mashabiki ambacho pia kilimpokea Harmonize.
.
Kusimamia wasanii kunamlia muda Alikiba kwa sababu si kazi rahisi, All in All nadhani Uongozi wa Konde Gang umejipanga kuhakikisha Msanii wao anafika mjini.
All the best Ibraah TZ
.
Insta: Fb: Twit: Sangu Joseph
#KijanaMzalendo #IloveTZ
Sent using Jamii Forums mobile app