Hati fungani (Dhamana za Serikali ) ni uwekezaji ambao mtu binafsi ama taasisi inaweka kwa serikali ama taasisi binafsi kwa kuikopesha fedha ama kuipatia fedha kwa riba.
Ni kama kuweka hela kwenye akaunti ya benki ya akiba(fixed deposit) ambapo unakua unapewa riba ya hela yako.
Kwa hiyo hati fungani zipo za serikali kuu, mashirika ama taasisi binafsi kama benki, taasisi nyingine za umma na binafsi.
Hiyo inatokea pale taasisi ama serikali inahitaji hela kwa ajili ya kutekeleza jambo flani na haina hizo hela kwa wakati huo, hivyo inatangaza kwamba inahitaji kukopeshwa kutoka kwa umma, inatangaza kiasi inachotaka kukopa na pia ni mkopo wa muda gani.
Zipo hati fungani za muda mrefu na za muda mfupi. Za muda mfupi huishia chini ya mwaka mmoja na za muda mrefu kuanzia miaka 2 na kuendelea. Za muda mfupi zinaitwa Bills na za muda mrefu zinaitwa Bonds. Hivyo huitwa Treasury Bills na Treasury Bonds kama zimetolewa na serikali ama Corporate Bills and Corporate Bonds kama zimetolewa na mashirika binafsi, munucipal bills and municipal bonds kama zinetolewa na halmshauri ama mamlaka za miji.
Hati Fungani hizi zina soko lake maalumu ya kutangaziwa na ili ushiriki kwenye kununua ama kuikopesha serikali (unanunua hati fungani, unapewa hati/karatasi wewe unnawapa hela) ni lazima kupitia kwa wakala, kuna mawakala ama taasisi za fedha wamesajiliwa kwa ajili ya kununulia watu hati, sio kila mtu mmoja mmoja anaweza kununua.
Sasa ukishanunua, kama umenunua ya muda mfupi, maana yake ule muda ukiisha unarudishiwa pesa yako yote na riba. Ya muda mrefu unakua unalipwa riba kwa nusu mwaka, kama uliweka milioni 10 na riba ni 10%, basi kila baada ya miezi 6 unawekewa laki 5 kwenye akaunti na miezi 6 mingine laki 5 hadi muda uishe unarudishiwa pesa yako yote hivyo unakua umefaidika na riba.
Kwenye riba hapo unatakiwa uelewe kwamba Bills hazina riba kama riba bali kinachotokea ni kwamba serikali ama alietangaza anakwambia nakuuzia shilingi 100 kwa bei ya shilingi 95 kwa muda wa mwaka mmoja na mwaka mmoja uliisha nakupa shilingi 100 ingawa wewe ulinipa shilingi 95. Kitaalamu wanasema 100 was sold at discount and paid at face value at maturity. Kwa uelewa wa kawaida hiyo 5 uliyolipwa tutaiita riba.
Kiwango cha kuanzia ni kuanzia elfu 10 kama hawajabadilisha.
Hakuna namna usilipwe, ile sio biashara ya kiswahili lazima utalipwa tu.
Hope nimekupa mwanga kidogo.