Hivi hatuwezi kupangilia miji yetu?

Hivi hatuwezi kupangilia miji yetu?

Charliemic

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2019
Posts
602
Reaction score
969
Nimezunguka maeneo mengi ya Dar es salaam kwa mtizamo wangu ni haukufanyiwa planning! Stendi za daladala vimetengenezewa msongamano mkubwa mno na kelele nyingi saana zisizokuwa na tija.

Mfano stendi ya mbezi mwisho na mbagala rangi wajasiriamali wameweka vibanda visivyo rasmi ili kufanya biashara, kila mmoja ameweka "loud speaker" ya aina yake inayotoa kelele, wahubiri nao wamejazana na spika zao kila mmoja na mahubiri yake ili mradi mwishoni wapewe chochote, honi za magari ya kila namna wapiga debe nao lukuki, boda boda na bajaji zimejazana!

Njia za watembea kwa miguu kutoka na kuingia stendi zimewekwa vibanda, hali inayopelekea watembea kwa miguu kupita kwenye njia za magari.

Yaani ni stressfull

Huu mtindo wa kila mmoja kujiwekea loud speaker udhibitiwe, wafanyabiashara watengewe maeneo rasmi ambayo ni rafiki!

Kama tumeamua stendi ndio sehemu ya biashara basi stendi zote ziwe na maeneo rasmi ya biashara

Naomba mliotembea maeneo mengine duniani je miji mingine ya nchi zilizoendelea ipo kama hii ya kwetu?

Hivi hatuwezi kuupangilia mji wetu huu?
 
Tutakapaiondoa com madarakani kila kitu kinawezekana.. Maana wamewekeza kwenye siasa na kuipa thamani kubwa kuliko taaluma na weledi
 
Back
Top Bottom