Hivi hawa wanaishiaga wapi?


Walimu sio wa kulaumiwa peke yao hapa. Consensus inasema kwamba elimu ya mtoto ni 30% Mwalimu, 30% Mzee, 30% Mtoto mwenyewe, na 10% ni bahati. Kwa hiyo wote hapa wanastahili lawama. Binafsi nafikiri wazee wetu wabebeshwe lawama zaidi kwa vile wengi hawajihusishi na elimu za watoto wao katika kiwango chochote. Katika jamii nyingi zenye wakali kama vile wahindi, wayahudi, wachina utaona wazee wao wanajihusisha sana na harakati za kila leo kuwasaidia watoto wao kufanikiwa kimasomo.

Kwa kweli hizo statistics za matokeo ya form IV haziko tofauti sana na nchi nyini za KiAfrica ukizivunja kwenye points. Labda ndio mila yetu waafrika kutegemea walimu kama ni walezi pia. Kama vile "Mwalimu" Nyerere alikuwa baba yetu wa Taifa. Alipofariki tumekuwa mayatima

¬K
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…