Elections 2010 Hivi hawa 'watoto' wa nyerere vipi?

Elections 2010 Hivi hawa 'watoto' wa nyerere vipi?

Gottee

R I P
Joined
Sep 7, 2008
Posts
174
Reaction score
2
Katika moja ya sifa ambazo Hayati Baba wa Taifa alijijengea ni kutokumbatia mambo ya kipuuzi yaliyokuwa yakifanywa na Viongozi. Bado sijasahau namna Mwalimu alivyozima jaribio la kuunda Serikali Tatu ambalo liliasiliwa na lile kundi maarufu la Wabunge likiitwa G55. Bado nakumbuka namna Mwalimu alivyomshinikiza Mzee Mwinyi kuwataka Waziri Mkuu wa wakati huo John Malecela na Katibu Mkuu wa CCM Hayati Horace Kolimba wajiuzulu kwa kushindwa kumshauri Rais na Mwenyekiti wa Chama. Bado sijasahu Mwalimu alivyomkomalia Mzee Mwinyi na bila kutafuna maneno na kumwambia yu dhaifu.

Tangu Mwalimu ametutoka tumekuwa tukishuhudia mihadhara kadhaa ikifanyika yote ni katika kukumbuka yale yote mema aliyokuwa akiyafanya. Binafsi nimekuwa najiuliza hivi ni kweli mihadhara hii ya kumkubuka Mwalimu ina TIJA yoyote kwa taifa hili au ni namna tu fulani ya KUJIKOMBA (sijui kwa nani?) au kutafuna fedha za wavuja jasho wa Tanzania.

Hilo halitoshi. Kubwa kabisa ambalo nimekuwa nalifuatilia ni hili la viongozi ambao walifanya kazi kwa karibu na Mwalimu ambao wengi wao ni wastaafu kwa sasa. Tunaambiwa viongozi hawa walifanya kazi kwa karibu sana na Mwalimu na ambacho tumekuwa tukitegemea ni wao angalau kwa kiwango fulani kufanana na Mwalimu. Yaa kwa sababu ukika karibu na waridi na wewe utanukia waridi. Kundi hili la viongozi limekuwa kimya kiasi kwamba ninajiuliza ni nani KAWAROGA.

Wakati Familia ya Kikwete, Familia ya Makamba na kina Kinana wakiendelea kuichafua nchi kwa gharama yoyote ile ikiwemo kupandikiza sumu ya udini, hawa ‘watoto’ wa Hayati Mwalimu wamekuwa kimya bila kujitokeza hadharani kukemea. Nabaki najiuliza kama leo Mwalimu angefufuka sijui wangemwambia nini.

Kuna hawa watu kama Joseph Butiku, Joseph Warioba, Salim Ahmed Salim, Cleopa Msuya, Benjamin Mkapa (huyu sishangai japo nawajibika kumtaja), John Malecela (Huyu naye!) Pius Msekwa (huyu ana gubu la kiume!), Hassan Nassoro Moyo na wengine wengi. Najiuliza hawa watu ukimya wao una lengo la kumkomoa nani? Wanataka kumkomoa Hayati Mwalimu? Wanataka kumkomoa JK? Wanataka kumkomoa Slaa? Wanataka kuikomoa CCM? Wanataka kuwakomoa Wananchi? Au wanafanya mchezo wa kuigiza? Hivi hawajui kwamba MCHEZO wao ndio MAUTI yetu?

Kwa hiki wanachokifanya akina JK, Shimbo, Tendwa, Makame na ‘wahuni’ wengine hawa ‘watoto’ wa Mwalimu hawaoni kwamba kinaweza kuja kumwaga damu? Hivi damu ya Watanzania ikimwagika watakuja kusema nini? Definitely hakuna mmoja wa wanafamilia wao atakayemwaga damu au ndio sababu wameamua kukaa kimya. Hivi kama tunaamini huko mbele kuna maisha kwa maana hiyo ipo siku tutakutana na Mwalimu, watamwambia nini walifanya kuendeleza amani na utulivu aliotuachia? Msekwa hadi leo huwa anatamba kwamba yeye ndio Kiongozi wa Kitaifa wa mwisho aliyeongea na Mwalimu kabla hajakata kauli. Hivi anaweza kutuambia haya yanayotokea ndiyo Mwalimu alimwambia?

Ndoa za kikriso kabla hazijafungwa kanisani huwa zinatangazwa kwa muda fulani ili kama kuna mtu ana pingamizi na ndoo hiyo kufungwa alipeleke kanisani. Si ajabu kumsikia Kasisi akisema, “Kwa mara ya tatu tunatangaza ndoa ya Bwna Wai Exi na Bibi Zedi Pii itakayofungwa hapa tarehe kadhaa, kwa yeyote mwenye pingamizi na ndoa hii ASEME SASA LAA SIVYO ANYAMAZE MILELE.

Mimi na waambia akina Warioba na wenzake ni muda wao sasa kutamka kuhusu mustakbali wa Uchaguzi wa Tanzania na hali ya baadaye ya Taifa hili aliloliasisi 'baba yao' Mwalimu Julius Kambarage Nyerere la sivyo WANYAMAZE MILELE.

Nawasilisha
 
Huwatakii mema wenzako wewe hv unamfahamu ........ kwa visasi!
 
Kuna hawa watu kama Joseph Butiku, Joseph Warioba, Salim Ahmed Salim, Cleopa Msuya, Benjamin Mkapa (huyu sishangai japo nawajibika kumtaja), John Malecela (Huyu naye!) Pius Msekwa (huyu ana gubu la kiume!), Hassan Nassoro Moyo na wengine wengi. Najiuliza hawa watu ukimya wao una lengo la kumkomoa nani?

Hao wote wamefikisha ujumbe wao wa KUMKATAA Mkwere - kwa KUKAA kimya kabisa na kujitenga kwenye kampeni zake. Mwenye akiri ataupata ujumbe wao.

Warioba na Butiku walishasema saaaana, lakini hakuna kilichobadilika.
 
......thaaaaaanks.....!!! Kweli kabisa kimya chao hawa kitasababisha tuikimbie nchi. JK na wenzake walijaribu kutumia ukabila kututenga kwa kuwashambulia upinzani wakashindwa, sasa wamehamia kwenye udini.
 
Consultant,

Kama lengo ni kumkataa Mkwere, kwa nini wasingetamka hadharani na kuwaeleza wananchi kwa nini hawamtaki Mkwere! Dalili zote zinaonesha Mkwere anataka kurudi kwenye Kiti kwa gharama yeyote ile iwayo ikiwemo kukiuka maadili ya uchaguzi na kumwaga damu. Huoni kwamba SAUTI yao ni muhimu sana kwa wakati huu kuliko wakati mwingine wowote. Hivi unaonaje baada ya uchaguzi na labda watu fulani kujitwalia madaraka kwa nguvu halafu Oktoba mwakani kwenye 'dithday' ya Nyerer wale Mwalimu Nyerere foundation wanaandaa mjadala wa Uchaguzi wa Tanzania wa 2010. Halafu Warioba au Salim anaibuka na kuanza kusema sisi tuliyaona matatizo hayo na ndio maana tuliamua kunyamaza kimyaaaaaaaa kwa raha zetu! Halafu barua inatoka 'kuzimu' imeandikwa na Mwalimu akimwambia Warioba, "Hongera mwanangu kwa kumchunia Mkwere hata kama amerudi kwenye kiti potelea pote" Hivi kweli.....
 
Back
Top Bottom