JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Wakati Serikali ikiwa katika mpango wa kununua mabasi mapya zaidi ya 100 kwa sababu zinazoelezwa kwamba ni jitihada za kuboresha mradi wa Mwendokasi, kuna jambo linashangaza, kuna mabasi inawezekana yanafika 50 au zaidi hayafanyi kazi, kwa zaidi ya miezi sita sasa, yapoyapo yamepaki tu.
Mabasi hayo mengi yapo eneo la Ubungo nyuma ya unapofanyika ujenzi wa mradi soko la Kimataifa la Biashara (EACLC), yamepaki na haijulikani nini kinaendelea juu ya mabasi hayo.
Nimeyaona hayo na nilipouliza ‘wenyeji’ wanaosimamia mchongo huo wanadai ni mabovu.
Hali hiyo inatokea wakati ambapo abiria wanaoutegemea usafiri huo wakiendelea kukutana na kadhia ya kukaa muda mrefu kwenye vituo kutokana na uchache wa magari ambayo yanafanya kazi.
Changamoto hiyo ya kukosekana kwa magari ya kutosha imekuwa ikipesababisha kero kwa abiria ambao wanajazana kwa wingi kwenye mabasi hasa nyakati za asubuhi na jioni jambo linaonekana kuwa hatarishi.
Changamoto hizo ambazo zinaendelea kujitokeza zimefanya nijiulize, kwamba magari hayo yaliyopo eneo la Ubungo mamlaka husika zimeshindwa kuyatengeneza ili yaendelee kutoa huduma.
Kama tumewaza kununua magari mengine lakini tuliyonayo takribani 50 hayatumiki kutokana na kudaiwa kuharibika, sasa hayo yatakayokuja yatakuwa salama kiasi gani? Huenda tukaja kushuhudia baada ya muda nayo yanapaki kama hayo mengine.
Kuna mambo mengi ya kujiuliza, mfano wakati mradi unaanzishwa wahusika hawakujua namna ya kukarabati mabasi husika hususani, kuwa na kitengo imara cha matengenezo endapo mabasi yakiharibika ikiwemo namna upatikanaji wa spea.
Ni mchakato gani wa wazi unaoendelea juu ya ukarabati wa mabasi hayo? Ni vyema kama yameharibika katika kiwango ambacho hakiruhusu matengenezo umma uelezwe, tuelezwe tumepata hasara kiasi gani na uzembe ulikuwa wapi na wahusika ni akina nani?
Nawaza tu endapo mradi huo mmiliki angekuwa ni Mtu wa sekta binafsi, angekubali kuona magari zaidi ya 50 ambayo yamenunuliwa kwa mabilioni ya pesa yamepaki tu. Mwekezaji gani angeruhusu hilo litokee?
Nashauri ufanyike uchunguzi au Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG afanye ukaguzi maalumu kuhusu mabasi hayo ili kubaini ukweli unaoendelea, tujue ni hasara kiasi gani mpaka sasa imepatikana na ikibainika kuna uzembe wahusika wawajibike.
Ikumbukwe mabasi hayo yalinunuliwa kwa pesa za walipa kodi, hivyo ni muhimu wahusika wakazingatia uwajibikaji ambao utaendelea kutoa hamasa kwa wananchi kuendelea kuchangia kodi ili kushiriki vyema katika kuleta maendeleo katika Nchi yao.
Japokuwa kuna uhitaji wa mabasi mengine zaidi, lakini kuingia sokoni kununua mabasi hayo bila kujua hatma ya magari takribani 50 yaliyopaki kwa zaidi ya miezi mitano inaibua kizungumkuti na maswali mengi, suala ambalo linaweza kutafsiriwa na baadhi ya Watu kwamba ni matumizi mabaya ya pesa za umma.