Hivi haya mashindano ya Ndondo Cup ni ya kuibua Vipaji au yanaibua Wahuni wa muda mrefu waliotukuka?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Niseme tu ukweli na bila kuficha au kuwa ' Mnafiki ' ninachokiona katika haya ' Mashindano ' ya Ndondo Cup si vitendo vya ' Kimaadili ' kabisa hasa katika ' Jamii ' yetu ambayo ilianza ' Kustaarabika ' miaka mingi huko nyuma wakati wa enzi za akina Babu na Bibi zetu.

Ama hakika ukisema uende kutizama ' mechi ' huko ukiwa na ama Mkeo au Mwanao tegemea kupata aibu kubwa na ' Kustaajabu ' kwani Vitendo vingi ambavyo nimekuwa nikiviona huko ( katika Viwanja mbalimbali ambapo mashindano haya yanafanyika ) nimekuwa nikiviona sana katika ' Vijiwe ' vya ' bangi / bange ' na kule ambako ' Njemba ' zingine huenda Kunywa Gongo, Wanzuki na Mataputapu.

Kinachonishangaza ' Upuuzi / Upupu ' huu unaendelea na naona sasa unazidi kujizolea ' Sifa ' na tayari umeshaanza kuharibu Kizazi / Jamii lakini Wahusika wakuu wa ufuatiliaji wa ' mienendo ' ya Maadili nchini ' wameunyuti / wamenyamaza ' tu wakidhani kwamba pengine ' Kizazi ' hiki kikiharibika huko mbele ya safari labda ' Vizazi ' vyao havitaguswa au kuathirika kwa namna moja au nyingine.

Napenda sana Mpira na achilia mbali tu kuwa nimeshakuwa ' Mchezaji ' mpira tena mzuri tu kwa Viwango vya Shule, Vyuoni na Kitaani na nawaheshimu mno ' Waandaji ' wa haya ' Mashindano ' hasa ' Makamarada ' wangu akina Shaffih Kajuna Dauda, Alex Luambano na wengineo wote ila nadhani hili la ' Nidhamu ' na ' Maadili ' inabidi waliangalie sana ikiwezekana waanze sasa au kwa misimu ijayo ili iweze kutuvutia Watu wengine kuhudhuria pamoja na Wanafamilia wetu.

Yafuatayo tu ni baadhi ya ' matukio ' ya kusikitisha na kushangaza ambayo kama ukibahatika umeenda kushuhudia ' mashindano ' haya ya Ndondo Cup huwezi kuyakosa:

  1. Mashabiki ' Masela ' Kunya ( kutoa haja Kubwa ) hadharani.
  2. Mashabiki ' Masela ' Kuoga mbele ya Wageni rasmi.
  3. Mashabiki ' Masela ' Kunyoa ' mavuzi ' yao hadharani.
  4. Mashabiki ' Masela ' Kushindanishana ' Mikuyenge / Mibolo ' yao mechi ikiendelea.
  5. Mashabiki ' Masela ' Kuvuta ' Sigara Bwege / Bangi / Puje / Jani ' hadharani.
  6. Mashabiki ' Masela ' Kushindana ' Kujamba ' hadharani huku mechi ikiendelea.
  7. Mashabiki ' Masela ' kuwaringishia ' Mikuyenge / Mibolo ' yao wale akina Dada wanaopita Kuuza vitu mule ambapo ' Mashabiki ' wameketi.
Uvunjifu mkubwa sana wa ' Maadili ' unaendelea katika hii michuano ya Ndondo Cup hivyo udhibiti wa haraka unahitajika kuweza ' Kuokoa ' hiki ' Kizazi ' na tukumbuke kuwa ' Wahenga ' walisema " Kinga ni bora kuliko tiba ".

Nawasilisha.
 
Binafsi sijaona ubaya wa haya mashindano
ila pia sijauona umuhimu mkuubwa katika lengo la kukuza japo kuna faida fulani upande wa pili ya kuleta umoja na kupunguza matukio ya unyang,ang,anyi
[HASHTAG]#HappyBirthdayToMe[/HASHTAG]
 
Masela n wakuwavumilia tu...upate ugen wa masela wawil katka geto lako ndio utajua nn nnachosema maana ya kuwavumilia tu

Hakuna anayekataa ' Usela ' hasa ukizingatia kuwa hata Mimi mwenyewe ni ' Msela ' vile vile ila huwa nina ' maeneo ' yangu ya kufanya ' Usela ' wangu na ' Kamwe ' siufanyi mbele ya ' Kadamnasi ' kama vile. Mkuu hawa ' Masela ' wa Ndondo Cup sijui huwa ' wanavuta ' nini au wanakula ' goma ' gani kwani ule wanaoufanya sasa siyo tena ' Usela ' bali ni ' Upopoma / Upumbavu ' uliotukuka.
 
in short ww huendag mpirani hayo ndo unayo yafuatagaaa kuangaliaaaa wanayofanyaa maselaaa sasa ww kama umefataa mpiraa kwann usiangaliee mpiraa tenaa kwanziaa leo ntaanza kwendsa kumbe kuna watu wanaonyeshana mikuyenge aiseeee asante saana katikaa vitu napendaa kuona ni mikuyengee.......sasa kama ww hupendi usiendeee mimi nime confirm from today nitaendaa kwa ajili ya hayo uliyo yataja ilaa ww muongo khaaa!mtu anajambaa unamsikia wakat mpiraa unaendeleaaa we kiboko ,tuliaa kwako fuaa boxer na socks huo muda unaoendaa uwanjani
 
lazima utofauti uwepo kati ya premier league na ndondo cup
huo ndio utamu wake

bora niangalie ndondo kuliko vpl
Watu wanataka kutuletea ffu kwenye ndondo, ligi itakufa hapohapo. Tuachieni ndondo bwana nyie wa maadili bakini hukohuko
 
Hao masela mwaka jana walikuwa na jukwaa lao kabisaaa, na majukwaa mengine mambo shwari sana.
 
Ungetumia muda mwingi kuangalia kabumbu uwanjani wala usingepata muda wakukerwa na masela.ukitaka shuhuli iwe na nafuu kidogo basi weka kiingilio kinachoeleweka
 
Masela mtuache mbona nyie mkiwa mnafanya mambo ya ushoga hatuongi acheni kuzingua wauni tuburudike na usela hatuachi ndondo cup waletee chama langu vijana rangers tabata 1
 
Mi sina tatizo na hao masela, najua ndio mambo ya mipira ya uswahilini! Shida yangu ni kuona timu zimejaza wachezaji wa ligi kuu na waliostaafu! Timu zingechezesha wachezaji wa miaka kati ya 17 hadi 20 naamini ingekuwa fursa tosha ya kuibua vipaji vingi!
 
Kijana unapenda kuangalia mikuyenge ya wanaume wenzako....we mwenzetu kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…