Hivi hii bodi ya mikopo wana maana gani?

Joined
Aug 17, 2012
Posts
16
Reaction score
1
wadau mimi nimechaguliwa chuo kikuu mlimani. Chaajabu nimeomba mkopo lakini nimepewa zero kabisa yani kwa ufupi ni hata hela ya kula wameninyima. Hapa nilipo familia tunamtegemea mama na nina wadogo zangu nao wanahitaji kusoma kwa hiko kitu kidogo anachopata mama. Sasa najiuliza kwamba juhudi zote pamoja na kumaliza shule kwa shida mwishowe ndo nimenyimwa mkopo kabisaaa. Hapa nimechanganyikiwa hata sijui nifanyeje nimeenda bodi ya mikopo hata ndani sikuruhusiwa kuingia. Sasa nifanyeje au labda nitumie ujuzi niliopata jkt kufanya yasiyofaa niweze kwenda chuo maana ndo kilichobakia. Sio siri Tanzania ni nchi yangu lakini kwa hali waliyoniweka hawa watu naichukia mpaka kufa daah
 

duh...mkuu pole inabidi tupeane pole tu maana mimi mwenyewe nimepiga government olevo nina 11 na alevo nina 9 nimepangiwa electrical engineering halafu sina mkopo sijui maisha ya chuo yatakuwa vipi aisee yani sijapata jibu mpaka sasa hivi
 
ila wadogo zangu wote mliokosa mikopo msikate tamaa jaribuni kuapeal na pia mkifika vyouni mtasaidiwa na viongozi wa serikali ya wanafunzi mpate haki yenu
 

pole sana ndugu yangu kwanza hata mimi najiuliza hawa bodi ya mikopo Tanzania ipo kwa jaili ya kina nani?kama sisi watoto wa masikini tunaomaliza shule za kata tunapata shida namna hii kweli. mimi hapa nimechaguliwa mzumbe sina baba wala mama na nimeweka viambatanisho vyote lakini hata meal wameninyima kisa nimemaliza 2004 na nimeingia kwa equivalent. jamani elimu kwa stahili hii tutafika jamaniii. na haya ndio maisha bora?tendeni haki jamani ndugu zetu wa bodi ya mikopo mnatunyanyasa sna watoto wa masikini tunajua mchezo wenu mnawapa watoto wa wakubwa hakuna kificho mwisho wenu na ufisadi wenu unakaribia tuu. Mungu yupo watu hamna hata hofu ya Mungu?
 

Mkuu jibu la swali lako ni Ijumaa tukutane wizarani
 
hii nchi ni kama ya watu fulani au kikundi fulani cha watu,,,ambao wao ndio wapo kwa ajiri ya kufaidi matunda ya nchi hii...national cake is being enjoyed by leaders,their children,relatives,and their friends.utazani nchi aina viongozi wa kukanusha na kupinga mambo hayo,,,,hatali sanaaaaaaaaaa,,,
 
ni kweli kabisa wadau hakika haki ya mtu ni lazma aipate wafanye wafanyavyo kitaeleweka tu mwaka huu
 

Kaka hivi wewe ni MNUBI SIMBA ? NA WASI WASI HUO MKUUUUU
 
Pole man,,2po pa1,,kupangiwa cozi yenye priority co lazima upate mkopo maana mi naingia 2ndd year petroleum engrng but nimenyimwa mkopo kwa mara nyingine tena,,hawa majamaa vimeo sana yan
 
Mkuu jibu la swali lako ni Ijumaa tukutane wizarani

tumeenda leo wizara na tumektana na naibu mkurugenzi hapo wizarani na tumeongea nae tumeacha majina na indx namba zetu kasema majibu watatoa juma tatu kwenye vyombo vya khabar,na kama hawatatoa hzo taratibu ni vp tutaenda chuo bila mkopo tunarudi wizarani jumanne sa nne khasubuhi wk ijayo.ni hayo
 
njooni ijumaa hakuna cha j4 wamekuwa wakitoa taarifa tofaut tofaut wengine ijumaa na wengine j4 wote ijumaa tukutane
 

Tumia mafunzo na uzalendo mliojifunza JKT ndio maana ya taifa kuwapeleka JKT kwa gharama kubwa ili kupunguza kudeka deka. Unadhani Nuhu angekuwa anamdekea Yehova angemaliza ku-construct meli kubwa namna ile..??
 

jamani kama imeandika hizo index, na siye atujaenda huko na hzo index atujaandika itakuaje kwa siye
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…