Hivi hii falsafa ya wakiume kuvaa suruali na wa kike kuvaa gauni ilitoka wapi?

Hivi hii falsafa ya wakiume kuvaa suruali na wa kike kuvaa gauni ilitoka wapi?

Mtetezi.com

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
3,134
Reaction score
3,584
Kuna mambo ambayo kwa harakaharaka kwa akili ya kibinadamu ukijiuliza unakosa majibu!.
Ukijaribu kuzunguka almost dunia nzima utagundua kuwa hii falsafa ni pana na bila shaka ina maana pana zaidi kwani kwa harakaharaka ungeweza kuwaza yakuwa mwanaume ndiye angepaswa avae gauni na mwanamke avae suruali kwani yupo katika hatari kubwa ya kubakwa, kuchunguliwa au kudhalilishwa akiwa amevaa gauni kiurahisi za kuliko akivaa suruali.

Au walifanya hivyo kwa nia mbaya ili kuwatumia kama chombo cha starehe wanawake ili waweze kuwachungulia, kuwadhalilisha na hatimaye kuwabaka kiurahisi?

Katika baadhi ya mabara kama bara hindu na Asia utaratibu wao ni wa kanzu lakini piga ua ndani atavaa kinachofanana na suruali na wanawake watavaa gauni au kinachofanana na gauni!!

Wanawake wa miaka ya sasa hupendelea kuvaa suruali zaidi kupita gauni kwani hujisikia huru kukaa, kutembea na hata kucheza huru zaidi wakiwa wamevaa gauni au skirt, ila kiuhalisia katika hao huwezi kumkosa na gauni au skirt moja hii ni wazi kwamba haya ndio mavazi yao!.

Wewe unawaza nini kuhusu falsafa hiyo ya mavazi na je inakuathiri vipi na kukufaidisha vipi?
 
Mi nadhani mambo mengine yapo by nature tu. Tukianza kujiuliza kila kitu kilianzia wapi tutachelewa sana. Au nyie endeleeni kufanya uchunguzi mtuletee mrejesho ngoja na sisi tulime tuealetee wachunguzi mle.
 
Hapo hamna falsafa, ila ni utofauti wa maumbile kati ya mwanaume na mwanamke hasa kwenye jambo la kutoa haja.
Mwanamke anapata tabu kutoa haja ndogo pindi akivaa suruali, ila anakuwa huru kujisaidia haja ndogo akivaa suruali, hivyo wahenga walibuni mavazi ambayo yanaendana na maumbile yetu.
Pia sababu nyingine ni kuonesha utofauti kati ya jinsia mbili ya mwanaume na mwanamke, ingawa kuna nchi kama india wanaume na wanawake wanavaa nguo za aina moja.
Ila kwa kinachoendelea sasa duniani kwa wanawake kupenda kuvaa suruali limekaa kishetani zaidi, kwani shetani akitaka kumpata mwanaume mwenye msimamo lazima atamtumia mwanamke kwa namna moja ama nyingine, pia kwa sasa mwanamke kuvaa suruali wanasema wanakuwa huru na usalama unakuwa mkubwa hasa kwa vitendo kama ubakaji
 
Haki sawa hata wewe unaweza kuvaa gauni mbona wanawake wanavaa suruali zetu
 
Baada ya evolution, yani kutoka nyani to binadamu sisi waafrika tulikua tunaziba nyeti zetu tu mwili mzima unakuwa wazi. Haya maupuuzi mengine yameletwa na ukoloni. Bora turudi tutokapo.
 
Mi siwazi, Waswahili wanavaa kanzu bila kitu ndani na wadada wanavaa suruali, pambaneni na hali zenu
 
Hapo hamna falsafa, ila ni utofauti wa maumbile kati ya mwanaume na mwanamke hasa kwenye jambo la kutoa haja.
Mwanamke anapata tabu kutoa haja ndogo pindi akivaa suruali, ila anakuwa huru kujisaidia haja ndogo akivaa suruali, hivyo wahenga walibuni mavazi ambayo yanaendana na maumbile yetu.
Pia sababu nyingine ni kuonesha utofauti kati ya jinsia mbili ya mwanaume na mwanamke, ingawa kuna nchi kama india wanaume na wanawake wanavaa nguo za aina moja.
Ila kwa kinachoendelea sasa duniani kwa wanawake kupenda kuvaa suruali limekaa kishetani zaidi, kwani shetani akitaka kumpata mwanaume mwenye msimamo lazima atamtumia mwanamke kwa namna moja ama nyingine, pia kwa sasa mwanamke kuvaa suruali wanasema wanakuwa huru na usalama unakuwa mkubwa hasa kwa vitendo kama ubakaji
Mbona unamsingizia shetani?
 
Uko hivi

Wanaume tunavaa suruali kwa sababu umbo la ubooo ni sawasawa na umbo la suruali (mguu wa suruali) na wanawake wanavaa sketi kwa sababu umbo la papuchi ni sawa na umbo la sketi.
Wahenga walikuwa majiniazi sana.
 
Ni kutokana na maumbile ya mwanamke katika makalio na hips.Hayawezi kusitiriwa vzur na suruali.
 
FALSAFA ya mwanamke kukojoa akiwa amechuchumaa na Mwanaume akiwa amesimama imetoka wapi?
 
Lakini ukiangalia nchi za mashariki ya kati, Afrika ya kaskazini na sehemu kubwa ya Asia wanaume huvaa kanzu au msuli na ni wanawake ndio wanaovaa magagulo yanayoteremka mpaka kisiginoni. Sehemu kama India na Pakistani wanawake wanavaa sari zao lakini ndani chupi zao zina miguu mirefu kama suruali. Ni mila na desturi tu kuwa ni kipi kinavaliwa na jinsia ipi.

Kwa kwetu sisi mila za wanawake kuvaa gauni au kanga nafikiri ilikuwa kuwarahisishia katika kujiweka usafi na kwenda msalani. Fikiria mwanamke alievalia suruali tabu anayopata kwenda haja ndogo ukifananisha na mwanaume.
 
Nilishawahi kufikiria hivo but nikaona haina maana kwangu kufikiria hivo huku niki-emagine vile nikivaa gauni takavo behave. Niliachana na hizo mambo kitambo.
 
Back
Top Bottom