Hivi hii ni kwangu mimi tu ama ni kwetu sote?

Cytochrome p450

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2019
Posts
5,638
Reaction score
15,044
Huwa inanitokea na ni kawaida yangu kila ninapofanya vizuri au kufanikiwa katika jambo fulani, basi natafuta namna yeyote ile ya KUJIPONGEZA.

Vile vile nikiwa nimeharibu au kukosea kwenye jambo lolote ambalo nahisi sikustahili kuharibu, basi huwa natafuta namna yeyote ya KUJIPOZA.

Mfano: Nikifanikiwa huwa natafuta sehemu moja iliyotulia sana, kisha nashusha misosi ya nguvu pamoja na vinywaji. Hali inakuwa hivyo hivyo pale ninapozingua.

Hivi hii imekaaje wakuu, ni kwangu mimi Tu au ni kwetu sote?

Tuambiane pia, wewe huwa unafanya nini pale zinapotokea hali zote mbili?
 
Mimi hata nikitoka kwenye harakati zangu za maisha tu, nikapata hata chakula tu; hasa ninapoingia geto tu huwa napomoka chini tu namshukuru Mungu. Ni mara nyingi.

Huwa nawaza " ni wangapi hawajapata msosi wa leo na pia wangapi hawana hata pamba za kujistiri na wangapi hawana hata geto, ukiachana na nyumba?

Huwa najiona kama Mungu kanionea huruma sana, maana wenye shida na matatizo ni wengi sana. Tena wenye maana kuliko hata mimi zaidi!
Naona kama nimependelewa na Mungu.

Thus why karibia kila siku namshukuru Mungu tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom