Elections 2010 Hivi hii sio rushwa katika uchaguzi?

Elections 2010 Hivi hii sio rushwa katika uchaguzi?

Mwanamayu

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2010
Posts
11,662
Reaction score
6,888
Katika kampeni za uchaguzi jimbo la Kawe, wananchi wa Kawe walimuuliza mgombea wa Chadema, Halima Mdee, ni kwa jinsi gani atawatatulia kero ya kufungwa kwa njia ya ‘short cut' kwa kutembea kwa miguu (si ya magari) na JWTZ kambi ya Lugalo? Njia hii ni kati ya ile ya Kawe kuungana na ile ya Ali Hassan Mwinyi/ New Bagamoyo Road – shortcut ni kutokea pale darajani kwenye barabara ya kuelekea Bagamoyo. Jeshi liliwalazimisha wananchi kufuata barabara ya magari. Halima Mdee aliwajibu wananchi kuwa wakimpa ridhaa ya uwakilishi, atafuatiliwa suala hilo kwa kuzingatia sheria kwa maana ya kuangalia mipaka ya ardhi – JWTZ Lugalo linamiliki eneo mpaka wapi kisheria.

JK alipofanya nae mkutano na wana-Kawe walimweleza kero hiyo na kusema kuwa atalifanyia kazi. Nijuwavyo mimi maana yake akipewa ridhaa ya kuwa Rais. Cha ajabu njia ile imekwisha funguliwa na wakazi wanaitumia na jana nimepita hapo nikiona watu wakipita. Sasa swali langu je, kuwaahidi wapiga kura kuwa mkinichagua nitalifanyia kazi suala lenu, halafu kabla ya uchaguzi unatumia madaraka yako ambayo unamalizia kutoa order ya kufungua njia bila kujali kama kisheria ni sahihi au si sahihi huko sio kutoa rushwa? Kwani hao wana-Kawe si watakuwa wamekwisha shawishika? Pamoja na kuwa katiba iliandikwa na ‘walevi' lakini je hiyo ni sahihi? Je, mgombea mwingine wa urais angeliweza kutoa order kama hiyo? Je, huko sio kutumia vibaya madaraka kama Amiri jeshi mkuu, rais? Chadema wametuomba kutoa hukumu kwani Tendwa, Lewis na Augustino wameshindwa! Na ninawahakikishia nyie wana-Kawe, uchaguzi ukipita na JK akashinda hiyo njia itafungwa tena kama lili soko la wiki liloanzisha katikati ya barabara ya Lumumba mwaka 2005, je leo hii lipo pale? Je, baada ya uchaguzi liliendelea kuwepo? Naomba tuchague mambo endelevu na sio ya msimu!!!

Atakayelishughulikia kisheria anafaa zaidi kwani ataleta suluhisho la kudumu kuliko huyu anayelishughulikia kisiasa kwa kutumia cheo na urafi wa madaraka na ubovu wa katiba.
 
Back
Top Bottom