Hivi hiki ndicho Kiingereza cha Profesa Ndalichako?

Unaona sasa unafikiri ukiwa unaongea lazima ufuate grammar? Kweli hujaelimika nafikiri ukielimika utajua kuwa lugha ya kuongea hawafuati grammar mkuu kama unavyofundishwa darasani
Watu sio waelewa wakati hata sie tunaongea hichi kiswahili ila kina makosa kibao na hatujui kama ni makosa ila kwenye kiingereza ndio tumekariri mi grammar hatari.
 
😀 🤣🤣🤣
 
Huwezi kuwa Professor kwa nchi ambayo Kingereza ndiyo medium of instruction halafu uongee broken English ya hivyo, sina maana uongee kama mzungu lakini atleast uongee kingereza cha kueleweka.
Sasa kama lugha uliyotumia kupata hiyo Phd inakushinda lazima tuwe na mashaka na usomi wako.
 
Yeye kawakilisha ujumbe na umeeleweka kitu kingine mjue huyo kasoma siku nyingi Sana saiz ashaanza kusahau muachen mama watu
 
hapana mkuu unapokuwa na hasira hala lugha hutokea, mie hujikuta naongea italiano napokorogwa na mtu
 
Yeye kawakilisha ujumbe na umeeleweka kitu kingine mjue huyo kasoma siku nyingi Sana saiz ashaanza kusahau muachen mama watu
chamsingi wachina wako inside, mangine hayana maana, hivi watu hawaamini mambo yamebadilika?
 
hapana mkuu unapokuwa na hasira hala lugha hutokea, mie hujikuta naongea italiano napokorogwa na mtu
We umesema unaonge Kiitaliano sasa yeye hapo kaonge Broken English na vocabularies za kutafuta wa torch
 
Sema mimi mtu ambae anahangaika na lugha isiyomhusu nashangaa sana ndalichako ni mtanzania huyo si mwengereza kiingereza cha nini kwake kwanza katumia utu kumuelekeza ivo ilitakiwa aambiwe kwa kiswahili na kutupwa ndani imeisha hiyo
 
We umesema unaonge Kiitaliano sasa yeye hapo kaonge Broken English na vocabularies za kutafuta wa torch
yaani mtu kalipwa 80m kwa ajili yakujenga temporary office? hata wewe english ingekuwa deleted kichwani
 
chamsingi wachina wako inside, mangine hayana maana, hivi watu hawaamini mambo yamebadilika?
Hapana la msingi siyo wachina kuwa ndani, la msingi hapa ni mashaka juu ya elimu yetu kama Professor anayesimamia elimu ambayo kaipata kwa kutumia Kingereza anazungumza broken ya hivi, vipi wengine huko wanaotoa elimu kwa watoto wetu wana hali gani?
Na je bado elimu yetu ni bora au ndiyo maana graduates wanashindwa kucompete na wenzao waliosoma nje hata hapo Kenya
 
Sasa ndio naelewa kwa nini Wizara yake inaboronga inavyoboronga. Ana PhD ya makaratasi lakini si kwenye ubongo.
Kwaiyo una maana kujua kiingereza ndio kuwa na akili? Kwaiyo watu wa mataifa mengine wasioongea kiingereza hawana ubongo? ACHA KUWA MTUMWA WEWE, JIKUBALI UTANZANIA WAKO!!
 
Sema mimi mtu ambae anahangaika na lugha isiyomhusu nashangaa sana ndalichako ni mtanzania huyo si mwengereza kiingereza cha nini kwake kwanza katumia utu kumuelekeza ivo ilitakiwa aambiwe kwa kiswahili na kutupwa ndani imeisha hiyo
Shida ni kwamba huo uprofesa kaupata kwa kutumia Kingereza kama lugha ya kufundishia na siyo kichina wala kiswahili...
 
yaani mtu kalipwa 80m kwa ajili yakujenga temporary office? hata wewe english ingekuwa deleted kichwani
Muanzisha thread kajikita kwenye lugha siyo maamuzi aliyo chukua ndalichako dhidi ya mchina... hapa tunajadiri lugha na wasiwasi wa usomi wake
 
Tatizo mnalinganisha vitu viwili ambavyo haviendani, Elimu na Lugha ni vitu viwili tofauti.... Mfano wafuate wachina wanaojenga SGR au flyovers, je wanajua kiingereza? Na je kutokujua kwao Kiingereza ndio kunawafanya wasijue ujenzi?
 
huyu mheshimiwa degree ya pili na tatu kasoma Canada, nadhani alighafirika tu
 
Tatizo mnalinganisha vitu viwili ambavyo haviendani, Elimu na Lugha ni vitu viwili tofauti.... Mfano wafuate wachina wanaojenga SGR au flyovers, je wanajua kiingereza? Na je kutokujua kwao Kiingereza ndio kunawafanya wasijue ujenzi?
nawewe ndio kopo kabisa, SGR wanajenga waturuki, lakini ujue kiingereza sio dili kiivyo, 34% tu ya watu duniani ndio huongea kiingereza. ureno spain ukienda unaongea kiingereza wala hawakuelewi
 
Tatizo mnalinganisha vitu viwili ambavyo haviendani, Elimu na Lugha ni vitu viwili tofauti.... Mfano wafuate wachina wanaojenga SGR au flyovers, je wanajua kiingereza? Na je kutokujua kwao Kiingereza ndio kunawafanya wasijue ujenzi?
Wale wamepata elimu yao kwa kichina huwezi washangaa Kichina kwao ndiyo lugha ya ufundishaji.
Sasa we ni professor umepata elimu kwa kingereza Sekondari mpaka chuo miaka ndenda rudi hadi ukawa profesa. halafu lugha uliyo tumia kupata hiyo elimu inakupiga chenga. Je hiyo elimu umeipataje kama siyo magumashi? Ndiyo maana maprofessor wwetu wanafanya mambo ya ajabu kwasababu elimu waliyo nayo ni elimu jina hawaelewi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…