Hivi hili neno la Kiingerza linatamkwaje?

Hivi hili neno la Kiingerza linatamkwaje?

Makanyaga

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2007
Posts
11,129
Reaction score
7,321
Neno GENUINE linatamkwa kama "JENUINI" au "JENYWINYI"? Kuna tangazo kwenye TV linanichanganya sana!
 
hilo tangazo linasemaje? weka clip yake hapa tuone.
 
linatamkwa JENUINI. kwani kwenye hilo tangazo wao wanalitamkaje?
 
Neno GENUINE linatamkwa kama "JENUINI" au "JENYWINYI"? Kuna tangazo kwenye TV linanichanganya sana!

Kwa Kingereza neno hili linatamkwa JEN-YU-IN. Basi, JENYUIN. (Hamna ile herufi 'i' ya mwisho).

Mimi ni mwingereza nami nafundisha lugha ya Kingereza kwa wageni katika shule ya kimataifa hapa Uingereza. Zaidi ya hayo ninajitahidi kuendelea kujifunza Kiswahili!
 
Nakumbuka kuna mzungu mmoja alisema sisi tunawasema wao neno " ng'ombe" hawawezi kulitamka vizuri. Yeye naye akaniambia na sisi neno "terrible" hatulitendei haki katika matamshi.Je hili neno "terrible" unajua kulitamka vizuri?Naamini wengi tunajua "word pronunciation" na hatujui "word stress" na hapo ndipo tofauti ya matamshi inaanza unapokutana na mzawa wa ile lugha inatokea kile tunachoita “lugha gongana”.
Wataalam wanashauri ni bora kuwa na "correct word pronunciation and word stress” kuliko kuwa na “correct word pronunciation but wrong word stress”.
 
Shukran MPENDWA789 Na mimi ninashida ya kujifunza kiingereza zaidi na ningependa kuja Uingereza kwa muda wa miezi miwili au mmoja kwa ajili hiyo tu,, wewe kama mwalimu utanisaidiaje ? ? kwa gharama yangu kila kitu ?
 
Asante Silicon Valley! Haina maana sana kuja Uingereza kwa miezi miwili au mmoja kwa ajili ya lugha - ni safari ndefu na gharama kubwa sana! Kuweka msingi mzuri na mwenye nguvu wa lugha ambao utadumu lazima kuwepo hapo Uingereza muda usiopungua miezi sita! Kama ukija ningefurahi sana tuonane, lakini mimi siwezi kukusaidia na gharama ye yote.

Sijui kama unapenda au kuweza kutumia internet kujifunza Kingereza, lakini kama ni hivyo, websites ifuatayo ni bora:
---------------------
Kwa English grammar hii inafaa kuliko nyingine kadiri nilivyoona:
ENGLISH PAGE - Online English Grammar Book (Bonyeza) Hapa ni index ya grammar.
Hii ni Homepage: Advanced English lessons (Bonyeza)
---------------------
Kusoma na kusikiliza Kingereza (at the same time) BBC Worldservice Learning English ni bora.
Learning English - General & Business English (Bonyeza)
Chini ya General & Business English menu, "6 Minute English" na "English at Work" hasa inafaa.

Learning English - Grammar, Vocabulary & Pronunciation (Bonyeza)
Chini ya "Grammar, Vocabulary & Pronunciation" menu, "The English we speak" hasa inafaa.

Website ya BBC infaa sana kwa sababu yapo mazungumzo (conversations) mengi ya Kiingereza ya kila siku na zaidi ya hayo unaweza kusoma na kusikiliza at the same time. Pia, kulia na juu ya webpage nyingi unaweza kufungua audio file na text file, au ‘kudownload' yote kwenye computer yako (ukiwa na computer!)! Lakini kama ukitaka kusoma na kusikiliza at the same time kwenye internet, lazima to right-click on the audio au text file and then to choose the option "open link in new window". Ndipo utafungua files mbili separately ili kusoma na sikiliza pamoja.
Sijui kama itakusaidia.
 
Nakushukuru sana Mpendwa 789 kwa maelezo yako ya kina pia na ushauri mzuri ulionipa nitaendelea kufatilia hizo websites zote, bado nitakupa feedback kupitia JF au kama utanipa email address yako ntashukuru pia,, Wakati mwingine kuja Uingereza tuna kuwa na malengo zaidi ya moja, lugha ni moja pili kutoa matongotongo machoni yaani KUTALII kwa kujifunza na mengine mengi,
 
Nakumbuka kuna mzungu mmoja alisema sisi tunawasema wao neno " ng'ombe" hawawezi kulitamka vizuri. Yeye naye akaniambia na sisi neno "terrible" hatulitendei haki katika matamshi.Je hili neno "terrible" unajua kulitamka vizuri?Naamini wengi tunajua "word pronunciation" na hatujui "word stress" na hapo ndipo tofauti ya matamshi inaanza unapokutana na mzawa wa ile lugha inatokea kile tunachoita “lugha gongana”.
Wataalam wanashauri ni bora kuwa na "correct word pronunciation and word stress” kuliko kuwa na “correct word pronunciation but wrong word stress”.

hivi hujamchanganya mwenzio? stress? hahahaha!
ninapata shida kutamka maneno haya "examine", "determine", "example", "connect", "correct"
 
Back
Top Bottom