Asante Silicon Valley! Haina maana sana kuja Uingereza kwa miezi miwili au mmoja kwa ajili ya lugha - ni safari ndefu na gharama kubwa sana! Kuweka msingi mzuri na mwenye nguvu wa lugha ambao utadumu lazima kuwepo hapo Uingereza muda usiopungua miezi sita! Kama ukija ningefurahi sana tuonane, lakini mimi siwezi kukusaidia na gharama ye yote.
Sijui kama unapenda au kuweza kutumia internet kujifunza Kingereza, lakini kama ni hivyo, websites ifuatayo ni bora:
---------------------
Kwa English grammar hii inafaa kuliko nyingine kadiri nilivyoona:
ENGLISH PAGE - Online English Grammar Book (Bonyeza) Hapa ni index ya grammar.
Hii ni Homepage:
Advanced English lessons (Bonyeza)
---------------------
Kusoma na kusikiliza Kingereza (at the same time) BBC Worldservice Learning English ni bora.
Learning English - General & Business English (Bonyeza)
Chini ya General & Business English menu, "6 Minute English" na "English at Work" hasa inafaa.
Learning English - Grammar, Vocabulary & Pronunciation (Bonyeza)
Chini ya "Grammar, Vocabulary & Pronunciation" menu, "The English we speak" hasa inafaa.
Website ya BBC infaa sana kwa sababu yapo mazungumzo (conversations) mengi ya Kiingereza ya kila siku na zaidi ya hayo unaweza kusoma na kusikiliza at the same time. Pia, kulia na juu ya webpage nyingi unaweza kufungua audio file na text file, au ‘kudownload' yote kwenye computer yako (ukiwa na computer!)! Lakini kama ukitaka kusoma na kusikiliza at the same time kwenye internet, lazima to right-click on the audio au text file and then to choose the option "open link in new window". Ndipo utafungua files mbili separately ili kusoma na sikiliza pamoja.
Sijui kama itakusaidia.