Kommando muuza madafu
JF-Expert Member
- Aug 30, 2022
- 3,216
- 7,254
Kuna hii Kero ambayo ipo maeneo Mengi nchini sijui wenzangu mliosafiri kwenye nchi za wenzetu kuna hali kama hiyo.
Kero hii ni za wamachinga, bodaboda, madereva wa tax, wapiga debe na maajenti wa mabasi. Leo nitaongelea madereva wa boda boda, wapiga debe na machinga kwenye mastendi ya mabasi.
Ni kweli vijana wamejiajiri katika hizo sekta na wanapata vipato vyao halali. Ni jambo jema na la kushukuru ila hili suala la kulazimisha watu kununua, kupanda au kuwapangia nauli watakavyo wao si jambo jema. Mfano, Leo nipo Msamvu stend, atakuja Machinga anauza nazi mwingine anauza mikate, miwani n.k anasema ununue kuikataa akakasirika. Ukigonganisha macho na Machinga hapa stendi anakuulizia kama unanunua bidhaa yake. Kuikataa anakukasirikia. Hii kitu ipo hata kwenye boda boda/bajaji, ukigonganisha naye macho tu anataka akupakie kwenye pikipiki/bajaji yake. Maajenti na wapiga debe nao ni hivyo hivyo. Ukigonganisha nao macho tu, shida.
Kimsingi hii ni Kero kwetu wasafiri/wapitaji kwa maana toka nitoe kwangu kuka stendi au kupita kituo cha Boda najua naenda wapi na kama ningekuwa na uhitaji wa boda au bajaji au hivyo vitu wanavyouza ningewaita na kununua au panda usafiri wao. Utakuta mtu anauza miwani ile ya watoto nawe upo busy na mambo yako anakupitishia usoni au anakugusa mgongoni ili akuuzie au anakuomesha na kukuita hadi uitikie kwa kile anachotaka huduma. Usipoitikia anaona umemdharau lakini utaitikia na kununua kila.kitu kwa kila mtu ili umridhishe aone hujamdharau?
Sijui wenzetu mliosafiri nje ya nchi kuna utaratibu kama huu wa kulazimishwa huduma pale tu unapogonganisha macho na watoa huduma? Please, wahusika ondoeni hii Kero kwetu.