Hivi huko Somaliland uchumi wao ukoje

Hivi huko Somaliland uchumi wao ukoje

Nsama

Senior Member
Joined
Jul 15, 2022
Posts
192
Reaction score
249
Nilikuwa huko mjini Twitter nikakutana na hizi picha kutoka kwa ndugu zetu wa pembe ya Afrika. Nimestaajabishwa na hayo mapesa.

Je shida ni sarafu kukosa nguvu au shida ni gani wadau?.
 

Attachments

  • 20220825_225711.jpg
    20220825_225711.jpg
    50.1 KB · Views: 27
  • 20220825_225707.jpg
    20220825_225707.jpg
    39 KB · Views: 25
  • 20220825_225702.jpg
    20220825_225702.jpg
    50.3 KB · Views: 24
Unafahamu sifa za hela kwanza
 
Hahaa, kwamba kubeba elf ishirini unahitaji mkokoteni badala ya wallet?
 
Hizo pesa zote ulizoona kwenye hiyo video, ukija Bongo unapeleka kwa mama wauza mihogo unawauzia kama kuni halafu Wanakupa elfu kumi.
 
Hizo pesa zote ulizoona kwenye hiyo video, ukija Bongo unapeleka kwa mama wauza mihogo unawauzia kama kuni halafu Wanakupa elfu kumi.
Jombaa, shilingi moja ya Somalia ni sawa na shilingi nne za Tanzania. 1 SO Shilling- 4 TShs. (1$- 567 SOS)
Somaliland wanayo sarafu yao pia, SL Shilling. 1$- 580 SLSh.
Tatizo ni kwamba kule $ zinauzwa sana kwenye 'black market', sio kwenye benki wala forex.
 
Hizo pesa ukitengenezea mkaa wa karatasi bongo unaweza pata pesa zaidi ya thamani ya hizo pesa
 
Hakuna vita huko?
Jombaa, Somaliland kuna amani ni eneo ambalo lilijitenga na nchi ya Somalia tangia vita viibuke Somalia mwaka wa 1991. Ila bado hawajapata 'recognition' rasmi kama nchi. Wenzao wakipigana wao walikuwa wanajiendeleza na wakimbizi wa kisomali walikuwa wanakimbilia 'nchi' hiyo, kwasababu wao hawakuguswa na vita hivyo.

Wale jamaa ni tofauti sana na wasomali wenzao kisa mkoloni aliyetawala huko alikuwa ni muingereza, sio muitaliano kama maeneo mengine yote ndani ya nchi ya Somalia. Nilizuru mji wao mkuu wa Hargeisa mwaka wa 2019 na sikuamini kabisa kwamba nilikuwepo ndani ya nchi ya Somalia. Kuzuri sana kule kuna hoteli na sehemu nzuri sana za kiutalii na kiasili wasomali wa huko ni wastaarabu sana na sio wabaguzi kama wenzao.
 
Back
Top Bottom