Hivi huku duniani ni nini kinaendelea?

Hivi huku duniani ni nini kinaendelea?

wa stendi

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2016
Posts
25,190
Reaction score
27,434
Ni swali dogo kama la mzaha hivi lakini ukiulizwa kwa haraka haraka unaweza kosa jibu au ukajibu kile unachokiona /waza.

Je!ukiulizwa hili swali utajibu nini.
 
Huyo anaeuliza kwanza ye yuko wapi..? Kama anauliza halafu yupo duniani hapahapa wa hivyo huwa tunawapiga makofi ya mdomoni tu anakaa kimya tunaendelea kunywa mvinyo mpk hapo atakuwa ameshaelewa ya kuwa duniani nini kinaendelea!
 
Ni swali dogo kama la mzaha hivi lakini ukiulizwa kwa haraka haraka unaweza kosa jibu au ukajibu kile unachokiona /waza.

Je!ukiulizwa hili swali utajibu nini.

Unahamu ya kula Tango lenye Chumviiii siioo
acha maswali ya Kibwege

#Haya Mzee Mpili Naee Kawa Star Tanzania>>>
 
Mambo yanazidi kuvurugika, imeanza kuwa kawaida mwanaume kuwa mwanamke wa mwanaume, na mwanamke kuwa mwanaume wa mwanamke.

Ibadani nako hali si shwari wachungaji wamefikia hatua ya kula kondoo huku wakiendelea kutuhimiza tutoe tubarikiwe, wapi imeandikwa baraka zinanunuliwa hilo swali labda tutajibiwa siku yule mwana wa mariamu akirejea.

Vyuo kila mwaka vinatema wahitimu nyomi lakini pa kuwaweka hakuna bali tunawasihi saana wajiajiri sijajua kama vile vyeti kama ndio mtaji wenyewe.

Kwa ufupi huku duniani kuko hivyo
 
Hilo swali linatakiwa liulizwe na mtu wa buswele vijijini huko ambae hana access na mitandao ya kijamii hana tv

Gazeti anakuja kuliona mjini
 
Back
Top Bottom