Mambo yanazidi kuvurugika, imeanza kuwa kawaida mwanaume kuwa mwanamke wa mwanaume, na mwanamke kuwa mwanaume wa mwanamke.
Ibadani nako hali si shwari wachungaji wamefikia hatua ya kula kondoo huku wakiendelea kutuhimiza tutoe tubarikiwe, wapi imeandikwa baraka zinanunuliwa hilo swali labda tutajibiwa siku yule mwana wa mariamu akirejea.
Vyuo kila mwaka vinatema wahitimu nyomi lakini pa kuwaweka hakuna bali tunawasihi saana wajiajiri sijajua kama vile vyeti kama ndio mtaji wenyewe.
Kwa ufupi huku duniani kuko hivyo