I stand to be corrected, mimi naufahamu mkongo wa taifa kama ifuatavyo;
Ni njia kuu (HIGH WAY) ya wa mawasiliano ya data na sauti/voice kupitia optic fibre cables (nyaya maalumu za plastic ambazo zinasafirisha mawimbi kwa speed, ujazo mkubwa na kwa gharama nafuu).
Njia hii inawezesha mawasiliano ya ndani ya nchi na nje ya nchi.
Ndani ya nchi:
Sasa badala ya kutumia madishi na minara kusafirisha mawimbi kutoka sehemu moja mpaka nyingine, unaweza kutumia mkongo huu wa Taifa..........madishi na minara ni gharama kubwa kununua na kumeneji lakini kupitia mkongo wa taifa ni nafuu zaidi.
Nnje ya nchi:
Huu mkongo wa taifa umeunganishwa kwenye mkongo wa baharini ambao na wenyewe ni kama huu isipokua wenyewe umepita baharini, ukiunganisha nchi zote duniani zilizopakana na bahari.
Zamani mawasiliano ya nje ya nchi yalikua yanafanyika kupitia satelite = ambayo ni gharama kubwa, ila sasa mkongo wa taifa unatu-unganisha na dunia kupitia mkongo wa baharini ambao ni nafuu.
Mkongo wa Taifa (NICTBB) ni mali ya serikali ya jamhuri wa muungano wa Tanzania ila unasimamiwa na kundeshwa na kampuni ya simu ya TTCL.
Mkongo wa baharini unamilikiwa na kuendeshwa na kampuni ya SEACOM na ESSy.
Faida za mkongo wa Taifa:
Kuwezesha telemedicine, e-education, e-government n.k kwa gharama nafuu.