Hivi huu ni ugonjwa gani??

Quinton Canosa

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2012
Posts
1,224
Reaction score
1,250
Habari Jamii Forum dokta
Kuna ugonjwa unamuandaa mtoto wa kaka yangu nashindwa kuuelewa yaani anatokwa na mapele makubwa sehemu za kidevuni,kwenye mikono kwenye kisogo na hata kwenye paji la uso ni mapele makubwa sana yankuja na kuondoka na muda mwingine ngozi ya huyu mtoto inakakamaa saana anakuwa kama ametembelewa na konokono ngozi yake inavyong'aa nimekwenda hospitali wanasema hakuna kitu na siku za hivi karibuni mjoto lake la mwili linapanda mpaka 39c sasa sijajua tatizo nini hebu naomba na wewe msaada na kama kuna dawa unaifahamu naomba nijulishe
 
Huko hospitali mlikokwenda wawape referral letter kwenda kwa mtaalamu wa ngozi dermatologist. Ikiwezekana kipande cha ngozi kikatwe na kupelekwa laboratory
Naumwa mlango wa kumezea chakula juu ya koo naamini sio matezi.. limenianza jana. Ni ugonjwa gani mkuu?
 
Hospital ndio jibu sahihi.
Lakini kwa uzoefu watoto wengi sana wanasumbiliwa na allergy.

Kama hayo mapele yanatoa usaha inaweza kuwa infection.

ANGALIZO: Haya maelezo yangu siyo ushauri wa daktari.
 
Kama allergy basi usiweke karanga ktk lishe ya mtoto.
Maziwa ya ng'ombe, karanga, blue band, na baadhi ya samaki husababisha allergy kwa baadhi ya watoto na kusababisha mapele, vijipu chungu, mafua, n.k.
 
mungu akubariki kaka
 
Mayai ya kisasa chunga sana.
Kingine mwambie shemeji asiwe anampa mtoto vitu vya supamarket haswa vyakula.jaribu kumtengezea mtoto vitu nyumbani nunua sokoni lishe zile changanya kasage mwenyewe!juisi za matunda usinunue zilizo tayari jaribu kumtengenezea mwenyewe.nasisitiza mayai ya kisasa usimpe mtoto kabisa
 
kwa kauzoefubkadogo hayo mavitu yanawapata sana watoto kipindi hiki cjajua tatizo haswa ila kaa mbali na aquatic foods dagaa samakibna vingine kama hvyo
 
Pole sana mkuu angalia sana kama unampatia samaki alafu kama unafanya hivyo isimpatir samak kwa kipind kifupi kama 2weeks
 
Ukosefu wa chakula Bora, chakula Bora ndicho kinachoongeza Kinga ya mwili kupambana na matatizo hayo.
 
Hizo kitu zilishamtokeaga dogo wangu, nilihangaika sana hadi dawa za asili lkn wapi. Mwisho wa siku nikaja pata dawa moja yaitwa ketoconazole. Vilipotea vyote mazima.
Ila nakushauri nenda kwa wataalam kwanz.
 
Hospital ndio jibu sahihi.
Lakini kwa uzoefu watoto wengi sana wanasumbiliwa na allergy.

Kama hayo mapele yanatoa usaha inaweza kuwa infection.

ANGALIZO: Haya maelezo yangu siyo ushauri wa daktari.

Ni kweli, usimpe Maziwa ya Ng'ombe na Bidhaa zote zitokanazo na Maziwa, Samaki wa Baharini (Sea Foods), Karanga na Bidhaa zake.
Mtoto wangu alikuwa na Matatizo haya pamoja na Kikohozi kilichokuwa akiponi. Nilipompeleka Hospitali walinipa masharti hayo na nakuhakikishia AMEPONA kabisa,sasa ana miaka 16
Kama allergy basi usiweke karanga ktk lishe ya mtoto.
Maziwa ya ng'ombe, karanga, blue band, na baadhi ya samaki husababisha allergy kwa baadhi ya watoto na kusababisha mapele, vijipu chungu, mafua, n.k.
 
Ni kweli.
Hata mimi watoto wangu wawili wamenisumbua sana kabla ya kujua tatizo lao la ngozi, mafua na kikohozi lilikuwa linatokana na allergy hasa karanga ma maziwa ya ng'ombe.

Blue band pia iliwatoa vijipu sana wakati fulani.

Sasa mtoto mmoja kakua hasumbuliwi na hivyo vitu kama mdogo wake.
 
Mpe mlo kamili dogo simamia zoezi mwenyewe usimwachie msichana wa kazi.. lkn pia mazingira ya joto kali hupelekea tatizo hilo.. ni uzoefu wangu tu wa kulea mm sio dr
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…