Kwema Wakuu,
Leo weekend niliamua kumpeleka Kijana wangu mdogo hospital akachekiwe masikio na pua maana wiki yote hii ana Mafua na analalamika masikio na pua vinamuwasha. Hii hospital inasifika sana kwa kutoa huduma nzuri kwa watu wanaosumbuliwa na Magonjwa ya Masikio, Pua na Koo (ENT). Niliwauliza watu wawili watatu tofauti na wote wakanielekeza hapo.
Kama kawaida kufika Mapokezi nikaambiwa Kufungua file ni Tshs 5,000/= na kumuona daktari ni 20,000/= nkasema poa tu, nshakutana na hivi viwango hospital mbalimbali. Nimekaa foleni kufika zamu yangu nikaitwa wakamchunguza pale kwa vipimo vyao na wakanionyesha kinachomsumbua dogo mpaka anawashwa.
Walimpaka dawa masikioni na puani, mwisho wakaniambia nikalipie kwa Cashier nipewe dawa zingine za kuondoka nazo. Kwa sie wahenga wa enzi hizo situation kama hii ilikua unapewa faili lako linaloonyesha Vipimo na/au uchunguzi wa Daktari na Dawa ulizoandikiwa unaenda navyo Chumba cha dawa. Ila kwa hapa haikua hivyo. Kila kitu kinafanywa kwa System/Computer, we unaenda tu kutaja jina lako.
Shida ilianza kufika pale kwa Cashier, naambiwa bili yangu ni 132,000/=. Niliwauliza ni ya nini hii hela yote? Mbona nyingi? Walinijibu kua zile huduma za kule ndani kwa Dokta ni 30,000/=, na 102,000/= iliyobaki ni ya Madawa ambayo itabidi niyanunue. Nilipigwa na Butwaa maana hata hiyo huduma ya kumpaka dawa hawakuniambia ni kiasi gani wala kuniuliza kama nitahitaji afanyiwe ama lah. Nikasema poa tu, nailipia tu kuondoa tabu.
Sasa shida ingine ikaja hizo dawa za 102,000/=, nimewaambia waniambie ni dawa gani hizo zinazofikia hiyo amount wakanijibu sio utaratibu wao kumtajia mteja dawa wanazompa. Nikawaambia hizo dawa si nikilipia watanipa nitaziona tu, why wasinionyeshe kabla, wakajibu kama nataka nizilipie ndio nizione. Niliwauliza hizo dawa wamepanga kunipa mimi kweli?Mbona wananibania nisizijue?
Baada ya Kubishana sana, wakaanza kuniambia kua pale kuna dawa ya mafua, dawa ya fungus, dawa ya kutuliza maumivu na ingine nimeisahau. Ikabidi tu nimpigie mtu anitumie tigopesa nitamrudishia next time nikazinunua zote. Na cha ajabu wanatoa EFD Receipt tu ambayo inatoa only total amount, not itemized.
Nimewaza hizi dawa kwanini hawataki wateja tuzijue kabla? Sasa wanatulazimisha tununue dawa kwa bei wanazotaka wao wakati kila mtu ana utashi wake? Kwanini Serikali isiwabane hawa tu wenye Mahospital wauze Dawa zao kwa bei ya kawaida inayokubalika? Kama Bei zao sio za kumuibia mteja, why wazifiche? Serikali inajua huu wizi wanaofanya hawa Jamaa?
Wahusika chukueni hatua kwenye hili swala, Huduma ya Dawa na Matibabu ni Jambo muhimu katika Jamii, tuibiane kwenye mambo