Hivi Huu Wizi katika Mahospitali Umehalalishwa?

Shakir

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2012
Posts
1,627
Reaction score
1,926
Kwema Wakuu,

Leo weekend niliamua kumpeleka Kijana wangu mdogo hospital akachekiwe masikio na pua maana wiki yote hii ana Mafua na analalamika masikio na pua vinamuwasha. Hii hospital inasifika sana kwa kutoa huduma nzuri kwa watu wanaosumbuliwa na Magonjwa ya Masikio, Pua na Koo (ENT). Niliwauliza watu wawili watatu tofauti na wote wakanielekeza hapo.

Kama kawaida kufika Mapokezi nikaambiwa Kufungua file ni Tshs 5,000/= na kumuona daktari ni 20,000/= nkasema poa tu, nshakutana na hivi viwango hospital mbalimbali. Nimekaa foleni kufika zamu yangu nikaitwa wakamchunguza pale kwa vipimo vyao na wakanionyesha kinachomsumbua dogo mpaka anawashwa.

Walimpaka dawa masikioni na puani, mwisho wakaniambia nikalipie kwa Cashier nipewe dawa zingine za kuondoka nazo. Kwa sie wahenga wa enzi hizo situation kama hii ilikua unapewa faili lako linaloonyesha Vipimo na/au uchunguzi wa Daktari na Dawa ulizoandikiwa unaenda navyo Chumba cha dawa. Ila kwa hapa haikua hivyo. Kila kitu kinafanywa kwa System/Computer, we unaenda tu kutaja jina lako.

Shida ilianza kufika pale kwa Cashier, naambiwa bili yangu ni 132,000/=. Niliwauliza ni ya nini hii hela yote? Mbona nyingi? Walinijibu kua zile huduma za kule ndani kwa Dokta ni 30,000/=, na 102,000/= iliyobaki ni ya Madawa ambayo itabidi niyanunue. Nilipigwa na Butwaa maana hata hiyo huduma ya kumpaka dawa hawakuniambia ni kiasi gani wala kuniuliza kama nitahitaji afanyiwe ama lah. Nikasema poa tu, nailipia tu kuondoa tabu.

Sasa shida ingine ikaja hizo dawa za 102,000/=, nimewaambia waniambie ni dawa gani hizo zinazofikia hiyo amount wakanijibu sio utaratibu wao kumtajia mteja dawa wanazompa. Nikawaambia hizo dawa si nikilipia watanipa nitaziona tu, why wasinionyeshe kabla, wakajibu kama nataka nizilipie ndio nizione. Niliwauliza hizo dawa wamepanga kunipa mimi kweli?Mbona wananibania nisizijue?

Baada ya Kubishana sana, wakaanza kuniambia kua pale kuna dawa ya mafua, dawa ya fungus, dawa ya kutuliza maumivu na ingine nimeisahau. Ikabidi tu nimpigie mtu anitumie tigopesa nitamrudishia next time nikazinunua zote. Na cha ajabu wanatoa EFD Receipt tu ambayo inatoa only total amount, not itemized.

Nimewaza hizi dawa kwanini hawataki wateja tuzijue kabla? Sasa wanatulazimisha tununue dawa kwa bei wanazotaka wao wakati kila mtu ana utashi wake? Kwanini Serikali isiwabane hawa tu wenye Mahospital wauze Dawa zao kwa bei ya kawaida inayokubalika? Kama Bei zao sio za kumuibia mteja, why wazifiche? Serikali inajua huu wizi wanaofanya hawa Jamaa?

Wahusika chukueni hatua kwenye hili swala, Huduma ya Dawa na Matibabu ni Jambo muhimu katika Jamii, tuibiane kwenye mambo
 
Kwema Wakuu,

Leo weekend niliamua kumpeleka Kijana wangu mdogo hospital akachekiwe masikio na pua maana wiki yote hii ana Mafua na analalamika masikio na pua vinamuwasha. Hii hospital inasifika sana kwa kutoa huduma nzuri kwa watu wanaosumbuliwa na Magonjwa ya Masikio, Pua na Mdomo (ENT). Niliwauliza watu wawili watatu tofauti na wote wakanielekeza hapo.

Kama kawaida kufika Mapokezi nikaambiwa Kufungua file ni Tshs 5,000/= na kumuona daktari ni 20,000/= nkasema poa tu, nshakutana na hivi viwango hospital mbalimbali. Nimekaa foleni kufika zamu yangu nikaitwa wakamchunguza pale kwa vipimo vyao na wakanionyesha kinachomsumbua dogo mpaka anawashwa.

Walimpaka dawa masikioni na puani, mwisho wakaniambia nikalipie kwa Cashier nipewe dawa zingine za kuondoka nazo. Kwa sie wahenga wa enzi hizo situation kama hii ilikua unapewa faili lako linaloonyesha Vipimo na/au uchunguzi wa Daktari na Dawa ulizoandikiwa unaenda navyo Chumba cha dawa. Ila kwa hapa haikua hivyo. Kila kitu kinafanywa kwa System/Computer, we unaenda tu kutaja jina lako.

Shida ilianza kufika pale kwa Cashier, naambiwa bili yangu ni 132,000/=. Niliwauliza ni ya nini hii hela yote? Mbona nyingi? Walinijibu kua zile huduma za kule ndani kwa Dokta ni 30,000/=, na 102,000/= iliyobaki ni ya Madawa ambayo itabidi niyanunue. Nilipigwa na Butwaa maana hata hiyo huduma ya kumpaka dawa hawakuniambia ni kiasi gani wala kuniuliza kama nitahitaji afanyiwe ama lah. Nikasema poa tu, nailipia tu kuondoa tabu.

Sasa shida ingine ikaja hizo dawa za 102,000/=, nimewaambia waniambie ni dawa gani hizo zinazofikia hiyo amount wakanijibu sio utaratibu wao kumtajia mteja dawa wanazompa. Nikawaambia hizo dawa si nikilipia watanipa nitaziona tu, why wasinionyeshe kabla, wakajibu kama nataka nizilipie ndio nizione. Niliwauliza hizo dawa wamepanga kunipa mimi kweli?Mbona wananibania nisizijue?

Baada ya Kubishana sana, wakaanza kuniambia kua pale kuna dawa ya mafua, dawa ya fungus, dawa ya kutuliza maumivu na ingine nimeisahau. Ikabidi tu nimpigie mtu anitumie tigopesa nitamrudishia next time nikazinunua zote. Na cha ajabu wanatoa EFD Receipt tu ambayo inatoa only total amount, not itemized.

Nimewaza hizi dawa kwanini hawataki wateja tuzijue kabla? Sasa wanatulazimisha tununue dawa kwa bei wanazotaka wao wakati kila mtu ana utashi wake? Kwanini Serikali isiwabane hawa tu wenye Mahospital wauze Dawa zao kwa bei ya kawaida inayokubalika? Kama Bei zao sio za kumuibia mteja, why wazifiche? Serikali inajua huu wizi wanaofanya hawa Jamaa?

Wahusika chukueni hatua kwenye hili swala, Huduma ya Dawa na Matibabu ni Jambo muhimu katika Jamii, tuibiane kwenye mambo
Sasa serikali itajuaje kama hata jina la hospital umelificha????
 
Kupigwa nje nje
Hata kwenye maswala Muhimu kama Afya tunaibiana yaani,
Umelipishwa hela za kutosha tu na mwishowe unapewa risiti ya EFD inayoonyesha jumla tu, sio kimoja kimoja,
Hivi hakuna kweli watu wa serikali wanaotibiwa kwenye hizi hospital wakatusaidie kuwapeleka kina [HASHTAG]#Faustine[/HASHTAG] Ndungulile na [HASHTAG]#UmmyMwalimu[/HASHTAG] kweli?
 
Taja hospitali sasa inajulikanaje??
 
Hospital zao hizo wengine wanahisa yanaingilia kushoto yanatokea kulia
 
Mimi huwa namuuliza daktari moja kwa moja baada ya majibu dawa gani ananiandikia kwa kisingizio kuwa Nina allergy na baadhi ya sawa, nikifika dirishani wakileta longolongo nduki naenda maduka ya dawa ya jumla na rejareja yana bei za discount .
 
Hata kwenye maswala Muhimu kama Afya tunaibiana yaani,
Umelipishwa hela za kutosha tu na mwishowe unapewa risiti ya EFD inayoonyesha jumla tu, sio kimoja kimoja,
Hivi hakuna kweli watu wa serikali wanaotibiwa kwenye hizi hospital wakatusaidie kuwapeleka kina [HASHTAG]#Faustine[/HASHTAG] Ndungulile na [HASHTAG]#UmmyMwalimu[/HASHTAG] kweli?
Hapo kwenye list isiyo na mchanganuo ndo penye ukakasi zaidi.
 
Hospital iko Nyuma ya Kituo Cha Mafuta cha Super Star pale Mwembechai,
Haina jina unafikiri kila mtu anayajua maeneo hayo. Kama kweli hujatendewa sana kwanini unaogopa kuitaja??
 
Kwema Wakuu,

Leo weekend niliamua kumpeleka Kijana wangu mdogo hospital akachekiwe masikio na pua maana wiki yote hii ana Mafua na analalamika masikio na pua vinamuwasha. Hii hospital inasifika sana kwa kutoa huduma nzuri kwa watu wanaosumbuliwa na Magonjwa ya Masikio, Pua na Koo (ENT). Niliwauliza watu wawili watatu tofauti na wote wakanielekeza hapo.

Kama kawaida kufika Mapokezi nikaambiwa Kufungua file ni Tshs 5,000/= na kumuona daktari ni 20,000/= nkasema poa tu, nshakutana na hivi viwango hospital mbalimbali. Nimekaa foleni kufika zamu yangu nikaitwa wakamchunguza pale kwa vipimo vyao na wakanionyesha kinachomsumbua dogo mpaka anawashwa.

Walimpaka dawa masikioni na puani, mwisho wakaniambia nikalipie kwa Cashier nipewe dawa zingine za kuondoka nazo. Kwa sie wahenga wa enzi hizo situation kama hii ilikua unapewa faili lako linaloonyesha Vipimo na/au uchunguzi wa Daktari na Dawa ulizoandikiwa unaenda navyo Chumba cha dawa. Ila kwa hapa haikua hivyo. Kila kitu kinafanywa kwa System/Computer, we unaenda tu kutaja jina lako.

Shida ilianza kufika pale kwa Cashier, naambiwa bili yangu ni 132,000/=. Niliwauliza ni ya nini hii hela yote? Mbona nyingi? Walinijibu kua zile huduma za kule ndani kwa Dokta ni 30,000/=, na 102,000/= iliyobaki ni ya Madawa ambayo itabidi niyanunue. Nilipigwa na Butwaa maana hata hiyo huduma ya kumpaka dawa hawakuniambia ni kiasi gani wala kuniuliza kama nitahitaji afanyiwe ama lah. Nikasema poa tu, nailipia tu kuondoa tabu.

Sasa shida ingine ikaja hizo dawa za 102,000/=, nimewaambia waniambie ni dawa gani hizo zinazofikia hiyo amount wakanijibu sio utaratibu wao kumtajia mteja dawa wanazompa. Nikawaambia hizo dawa si nikilipia watanipa nitaziona tu, why wasinionyeshe kabla, wakajibu kama nataka nizilipie ndio nizione. Niliwauliza hizo dawa wamepanga kunipa mimi kweli?Mbona wananibania nisizijue?

Baada ya Kubishana sana, wakaanza kuniambia kua pale kuna dawa ya mafua, dawa ya fungus, dawa ya kutuliza maumivu na ingine nimeisahau. Ikabidi tu nimpigie mtu anitumie tigopesa nitamrudishia next time nikazinunua zote. Na cha ajabu wanatoa EFD Receipt tu ambayo inatoa only total amount, not itemized.

Nimewaza hizi dawa kwanini hawataki wateja tuzijue kabla? Sasa wanatulazimisha tununue dawa kwa bei wanazotaka wao wakati kila mtu ana utashi wake? Kwanini Serikali isiwabane hawa tu wenye Mahospital wauze Dawa zao kwa bei ya kawaida inayokubalika? Kama Bei zao sio za kumuibia mteja, why wazifiche? Serikali inajua huu wizi wanaofanya hawa Jamaa?

Wahusika chukueni hatua kwenye hili swala, Huduma ya Dawa na Matibabu ni Jambo muhimu katika Jamii, tuibiane kwenye mambo
Hahaha mkuu hujaibiwa ila umeenda kwenye hosiptali ambayo inazidi uwezo wako...
Wewe ni sawa na mtu anayelalamikia kukuta selena hotel soda ni sh 2000 wakati bei elekezi ni sh 500..

Kuna hosiptali kulingana na hadhi yake hata panado sio sh 50 tena..

Kwahio siku nyingine uwe unaenda zahanati tu kutibiwa maana sekta ya afya ni biashara kama biashara nyingine na wala sio sehemu ya charity..

Kuhusu kupewa dawa usizozijua hapo nakiri wamekosea kwenye ethics za kidaktari ..huwezi kumpa mgonjwa matibabu ambayo hayajui na hajakubaliana nayo..kwa hapo wamekosea lakini kwa bei ni sawa kabisa kulingana na hadhi ya hisiptali yenyeww
 
Kuna dispensary ndogo alilazwa ndugu yangu,alipata tumbo la kali la kuhara.Alienda hospital sa 5 usiku,nmefika asubuhi pale napewa bill ya elfu 75 wakati dawa wamempa hata hazieleweki wakampa na oral ya kunywa basi.
 
Dah!
 
Mimi huwa namuuliza daktari moja kwa moja baada ya majibu dawa gani ananiandikia kwa kisingizio kuwa Nina allergy na baadhi ya sawa, nikifika dirishani wakileta longolongo nduki naenda maduka ya dawa ya jumla na rejareja yana bei za discount .
Hapo labda sawa Mkuu,
Ila kwa wale wa pale nadhani watakuambia uawatajie hizo dawa ambazo una allergy nazo ili wasikuandikie, lakini still wao za kwao hawatokutajia
 
Hahaha mkuu hujaibiwa ila umeenda kwenye hosiptali ambayo inazidi uwezo wako...
Wewe ni sawa na mtu anayelalamikia kukuta selena hotel soda ni sh 2000 wakati bei elekezi ni sh 500..

Kuna hosiptali kulingana na hadhi yake hata panado sio sh 50 tena..

Kwahio siku nyingine uwe unaenda zahanati tu kutibiwa maana sekta ya afya ni biashara kama biashara nyingine na wala sio sehemu ya charity..

Kuhusu kupewa dawa usizozijua hapo nakiri wamekosea kwenye ethics za kidaktari ..huwezi kumpa mgonjwa matibabu ambayo hayajui na hajakubaliana nayo..kwa hapo wamekosea lakini kwa bei ni sawa kabisa kulingana na hadhi ya hisiptali yenyeww
Nielewe Mkuu,
Mimi sijalalamika kua bei kua ni kubwa,
Bali nimesema nimetajiwa bei bila kufahamishwa ni dawa zipi hasa zenye hiyo Bei,
Hizo Dawa walizonipatia wangefahamisha ni dawa gani, na kila moja ni bei gani ili nijue nalipia nini,
 
Hiyo ni biashara kama biashara zingine waliogopa kukutajia jina la dawa huenda ungekwenda kununua sehem nyingine wakati wao wamefanya uchunguzi na kugundua dawa itakayo mfaa dogo
Pole lakini kama ulikuwa hujajipanga lazima utamaind tu
 
Kwema Wakuu,

Leo weekend niliamua kumpeleka Kijana wangu mdogo hospital akachekiwe masikio na pua maana wiki yote hii ana Mafua na analalamika masikio na pua vinamuwasha. Hii hospital inasifika sana kwa kutoa huduma nzuri kwa watu wanaosumbuliwa na Magonjwa ya Masikio, Pua na Koo (ENT). Niliwauliza watu wawili watatu tofauti na wote wakanielekeza hapo.

Kama kawaida kufika Mapokezi nikaambiwa Kufungua file ni Tshs 5,000/= na kumuona daktari ni 20,000/= nkasema poa tu, nshakutana na hivi viwango hospital mbalimbali. Nimekaa foleni kufika zamu yangu nikaitwa wakamchunguza pale kwa vipimo vyao na wakanionyesha kinachomsumbua dogo mpaka anawashwa.

Walimpaka dawa masikioni na puani, mwisho wakaniambia nikalipie kwa Cashier nipewe dawa zingine za kuondoka nazo. Kwa sie wahenga wa enzi hizo situation kama hii ilikua unapewa faili lako linaloonyesha Vipimo na/au uchunguzi wa Daktari na Dawa ulizoandikiwa unaenda navyo Chumba cha dawa. Ila kwa hapa haikua hivyo. Kila kitu kinafanywa kwa System/Computer, we unaenda tu kutaja jina lako.

Shida ilianza kufika pale kwa Cashier, naambiwa bili yangu ni 132,000/=. Niliwauliza ni ya nini hii hela yote? Mbona nyingi? Walinijibu kua zile huduma za kule ndani kwa Dokta ni 30,000/=, na 102,000/= iliyobaki ni ya Madawa ambayo itabidi niyanunue. Nilipigwa na Butwaa maana hata hiyo huduma ya kumpaka dawa hawakuniambia ni kiasi gani wala kuniuliza kama nitahitaji afanyiwe ama lah. Nikasema poa tu, nailipia tu kuondoa tabu.

Sasa shida ingine ikaja hizo dawa za 102,000/=, nimewaambia waniambie ni dawa gani hizo zinazofikia hiyo amount wakanijibu sio utaratibu wao kumtajia mteja dawa wanazompa. Nikawaambia hizo dawa si nikilipia watanipa nitaziona tu, why wasinionyeshe kabla, wakajibu kama nataka nizilipie ndio nizione. Niliwauliza hizo dawa wamepanga kunipa mimi kweli?Mbona wananibania nisizijue?

Baada ya Kubishana sana, wakaanza kuniambia kua pale kuna dawa ya mafua, dawa ya fungus, dawa ya kutuliza maumivu na ingine nimeisahau. Ikabidi tu nimpigie mtu anitumie tigopesa nitamrudishia next time nikazinunua zote. Na cha ajabu wanatoa EFD Receipt tu ambayo inatoa only total amount, not itemized.

Nimewaza hizi dawa kwanini hawataki wateja tuzijue kabla? Sasa wanatulazimisha tununue dawa kwa bei wanazotaka wao wakati kila mtu ana utashi wake? Kwanini Serikali isiwabane hawa tu wenye Mahospital wauze Dawa zao kwa bei ya kawaida inayokubalika? Kama Bei zao sio za kumuibia mteja, why wazifiche? Serikali inajua huu wizi wanaofanya hawa Jamaa?

Wahusika chukueni hatua kwenye hili swala, Huduma ya Dawa na Matibabu ni Jambo muhimu katika Jamii, tuibiane kwenye mambo
Ndg yangu kuepuka yote haya ungemkatia tu mwenetu toto afya kadi kutoka nhif anapata hiding za matibabu kwa mwaka mzima kwenye vituo zaidi ya 6000 Tanzania mzima
Unachotakiwa kuwa nacho ni picha ya passport size ya mtoto, nakala ya cheti cha kuzaliwa pamoja na mchango wa tsh 50400/= tu mkuu
 
Ahsante Mkuu,
Anayo hiyo kitu, sema ndio ime expire last week nikiwa niko safari.
So kesho Panapo Majaaliwa nitaenda kumkatia
 
Hiyo ni biashara kama biashara zingine waliogopa kukutajia jina la dawa huenda ungekwenda kununua sehem nyingine wakati wao wamefanya uchunguzi na kugundua dawa itakayo mfaa dogo
Pole lakini kama ulikuwa hujajipanga lazima utamaind tu
Hivi Mkuu haiwezekani ukaenda kufanya check up kisha ukigundua matatizo basi uanze kujipanga kutafuta hela ya kulipia?
Yaani ni lazima Check up wafanye wao na dawa pia wauze wao?
Sasa Pharmacy si zipo?
 
Kijana kama yuko below 18 yrs mkatie bima ya NHIF kwa 50400 tsh pekee ndani ya siju 20 za kazi unapata kadi ..Hutopata tena hizi kesi
 
Back
Top Bottom