GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Yaani watu wamefariki kwa ajali ya mitumbwi Ziwa Victoria huko Bunda Mkoani Mara wakienda Kanisani kumuabudu Mwenyezi Mungu, Mkuu wa Wilaya ya Bunda kaamuru Mchungaji wa Kanisa akamatwe haraka.
Kwanini GENTAMYCINE nimesema huenda huyu DC wa Bunda Dk. Vicent Kichwani mwake hazijakamilika?
Jibu lake lipo katika hii nukuu, "Nimeamuru Jeshi la Polisi likamkamate upesi Mchungaji wa Kanisa ambalo marehemu hawa walikuwa wakienda kusali. Kwanini alikuwa hakagui hiyo mitumbwi ili kuihakikisha kama iko salama kusafirisha waumini wake?
Na kwanini Kanisa lake liwe mbali huko kisiwani na asingelijenga huku Bunda Mjini?" Mkuu wa Wilaya ya Bunda Dk. Vicent Asubuhi hii ya leo akiwa anahojiwa moja kwa moja na Mtangazaji wa Redio ya Magic FM katika Kipindi chao kizuri cha morning magic.
Tafadhali aliye karibu na huyu DC hopeless wa Wilaya ya Bunda Dk. Vicent aniulizie kwake haya maswali yangu kwa niaba;
1. Je, juzi akiwa kama DC ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kusikia kuwa kuna Kanisa huko Kisiwani?
2. Je, ni jukumu la Mchungaji kuhakikisha usalama wa abiria wa ziwani au ni la Serikali na Mamlaka yake (zake) ndizo zenye Wajibu mkubwa?
3. Je, juzi ajali ilipotokea ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa DC huyu wa Bunda kujua kuwa kuna wananchi wake wanavuka Maji ya Ziwa Victoria kwenda kuabudu huko ng'ambo?
4. Je, huyu DC angepambana kuiomba Serikali Kuu kupitia kwa Boss wake Rais Samia kuwa kununuliwe kivuko kikubwa isingekuwa tiba kuu ya kuondokana na majanga haya na ajali hizi?
5. Je, huyu DC kusingetokea hii ajali na hali kuendelea kuwa shwari kwa usafirishaji ziwani angekurupuka na maamuzi haya haya ya kutaka Mchungaji akamatwe?
6. Je, tukisema kwake DC kuwa kwa kuamuru kwake kukamatwa kwa Mchungaji wa Kanisa hilo ni kama vile anataka kulazimisha na kuhamishia lawama kwa Mchungaji na Kanisa ili kuilinda Serikali na Idara zake ambazo kwa wenye akili ndiyo tunaona wana makosa/mapungufu?
7. Je, yeye kama DC tena mwenye Doctorate (PhD) yake akijipima anajiona ana akili timamu au hajabarikiwa nazo tokea azaliwe?
Mwisho tu GENTAMYCINE nimuombe Rais Samia kuwa siku zingine akiwa anateua wasaidizi wake wa ngazi mbalimbali awe ananialika Magogoni au Chamwino au Zanzibar ili niwe namsaidia, kwani nimeanza kugundua kuwa kuna wengine ni wajinga (pamoja na Kuvaa kwao suti) na anawateua kimakosa.