Nimevumilia nimeshindwa sasa nimeamua kusema very objectively ili wanaohusika ambao najua huwa wanapita huku wachukue hatua stahiki kutuondolewa kadhia hii kwani si kilema. Nimekuwa nakereka kweli nimuonapo huyu mama anaposoma hotuba za kithungu, hana vituo, anaongea kama yuko peke yake hadhira hana muda nayo kabisa, yuko speed kiasi anakosea hata maneno ya kawaida kabisa. Mwaka wa nane huu sasa hili halifanyiwi kazi wakati si kilema linarekebishika kirahisi kabisa. Mnaohusika mna mpango gani na hili? Ni sawa kwenu tukaendelea kudhalilishwa kwa jambo lililo ndani ya uwezo wetu? Mods itazameni post hii kwa upana wake msikurupuke na kuiondoa pasi na kuangalia mantiki yake. Ninaipenda nchi yangu kwa dhati kabisa ndio maana nimeliandika hili kwa nia ya kujenga si kubomoa.