Hivi Ibra Nation anakosea wapi?

Hivi Ibra Nation anakosea wapi?

kwa-muda

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2018
Posts
2,097
Reaction score
5,348
Kama kuna watunzi wazuri ambao wamewaandikia wasanii wengi na nyimbo zikawa hit akiwemo Maua Sama, akina Nandy na wengine wengi tu ni Ibra Nation.
Watu wengi wamemjua kwa wimbo wake wa Nilipize, japo hapo katia ametoa nyimbo kadhaa na sasa wimbo wake wa Tabibu lakini jamaa hatoboi.
Kila mtu anakubari kwamba jamaa ni mwandishi mzuri na anaowaandikia wanatoboa lakini yeye anatoa nyimbo nzuri lakini hapenyi.
Jamaa ana sauti nzuri ana melody nzuri lakini ameshindwa toboa sijui kwasababu gani. Huwezi sema anabaniwa maana alikuwa kwenye circle ya clouds kwenye zile studio ambako wakina nandy wanafanyia mziki na maproducer kama ringtone, kimamba, na wengine.
 
ngumu sana kujua...ila nahic kutoboa kunaendana na mind set ya mtu..mipango pamoja na mwonekano.
by the way ibra ni msanii mzuri sana
 
weka
Kama kuna watunzi wazuri ambao wamewaandikia wasanii wengi na nyimbo zikawa hit akiwemo Maua Sama, akina Nandy na wengine wengi tu ni Ibra Nation.
Watu wengi wamemjua kwa wimbo wake wa Nilipize, japo hapo katia ametoa nyimbo kadhaa na sasa wimbo wake wa Tabibu lakini jamaa hatoboi.
Kila mtu anakubari kwamba jamaa ni mwandishi mzuri na anaowaandikia wanatoboa lakini yeye anatoa nyimbo nzuri lakini hapenyi.
Jamaa ana sauti nzuri ana melody nzuri lakini ameshindwa toboa sijui kwasababu gani. Huwezi sema anabaniwa maana alikuwa kwenye circle ya clouds kwenye zile studio ambako wakina nandy wanafanyia mziki na maproducer kama ringtone, kimamba, na wengine.
Picha yake plz
 
Kwa kweli hata mimu huwa nashindwa kujua huyu jamaa anageli wapi kwa kweli. Labda hajaweza bado kujibrand, labda.
 
Sema angepewa promo kama la mtoto wa Gadner maana yule mtoto kapelekwa hata Fiesta wakati kuna wakali zaidi yake nadhani Ibra angepata promo la hivyo angetisha
 
Tatizo kila mtu anataka kuwa msanii akiendelea kuwa andikia kwa makubaliano Fulani nn kitaharibika?
 
Alianza kwa kuimba kabla ya kuwaandikia na wimbo wake ulikuwa mzuri na bado nyimbo zake ni nzuri sana.
Kuandika nyimbo Tanzania hakulipi ebu fikiria kama Nandy na Aslay walikuwa wamewapatia Tshs 300,000 waimbaji wa wimbo wa Subakheri ili waurudie na kuptia huo wimbo wao wakapiga show kibao wakapata deals za ubarozi na makampuni kibao si unyonyaji huo. Japo baadae kundi liliwageuka kuwa ule wimbo ni wa kundi si wa waimbaji inasemkana waliongeza mzigo ukafika milion na point lakini bado ni ndogo.
kama watayarishaji mziki wanatengeneza hits lakini bado hawana ela ebu fikiria mtu kama Esto keys sijui nimepatia jina, nilishangaa anasema studio yake ya mziki aliyoifungua kajibana sana ametumia ela nyingi sana kakusanya sana kiasi cha milion8, nikajiuliza huyu mtu katengeneza hits kibao yani ukisikiliza ngoma 10 ambazo ni hit kwa sasa hukosi nyimbo zake 5-6 inabidi awe na ela nyingi tu.
Waandishi hawapewi ela unakuta wanaandika tu kishikaji au bure kabisa, Marioo juzi ndipo kasema ameacha kuandika ila tu kwa makubariano kama mtu anataka amwandikie mfano wakubariane huu wimbo utakula show na kwingine mimi niachie ela ya caller tune na vitu kama hivyo lakini wasanii hawataki kusikia hizo habari.
Wasanii wanalalamika wananyonywa ila nao wanawanyonywa ma producer na waandishi. Marehemu Pancho alisema B-hits iliacha kuhit baada ya wasanii kutangaziwa kuwa kwasasa itabidi walipe hawafanyi tena nyimbo kishikaji.
 
Haya mambo ya kuzinduka huja kidogo kidogo, wameanza wasaanii kuzinduka zinduka na wengine watafuata hivyo hivyo taratibu.
 
Huyu mwamba anadai hana menejiment, pia mambo ya promo
 
Back
Top Bottom