Hivi Ina maana kuchimba chuma wenyewe ndio imeshindikana

Hivi Ina maana kuchimba chuma wenyewe ndio imeshindikana

Mechanic 97

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2021
Posts
854
Reaction score
1,296
Naandika Kwa masikitiko makubwa mno yaani vitu ambavyo vimefanywa miaka ya nyuma (1300) Huko China na (1650) na wenzetu wa ulaya. Kesho kutwa 2/8/2024 viongozi wa CCM. Wanaenda kusaini mikataba huko mundindi Ludewa Kwa ajili ya uchimbaji wa madini hayo na uchakataji na bila shaka ni kampuni ya kichina na Wamefanya hivyo Bila hata ya kuwapa nafasi wazawa Wenda wakapata kufunguka kwa kuwa njia ya uchukuzi/barabara inakwenda kukamilika na sijui wanafanya hivi kabla ya hata barabara kukamilika ili kuwawahi wa Tz au laaa sijui yaani.

Mimi navyo fahamu uchimbaji wa madini na uchakati wa madini ya chuma na makaa ya mawee huko liganga ulisubiri tuu barabara Kwasababu haitaji teknolojia ya hali juu sana. Kutokana teknolojia ya hali inatumika pale ambapo makaa ya mawee yanakua gharama ndio hapo utahitaji tanuli la upepo wa moto (blast furnace). Lakini Kwa upande wa ludewa makaa ya mawe yapo jirani hivyo unaweza anza hata Kwa tanuli ndogo kabisa na za kawaida na kuna mwenzetu huko ludewa Mzee Kisangani kasha jaribu na alitegemeea vijana wengine kama 200 waingie.


Mimi pia nilitegemea makundi ya vijana wadogo na wa makamo kutoka pande zote za nchi wakiwamo (wasomi, mafundi, wajasiriamali na etc) wataungana pamoja na Mzee Kisangani pindi tu barabara itakapo kamilika watakwenda kufanya Moja Kwa Moja shughuli zilipo kwenye makaa ya mawee na chuma sio kuwa manamba, sijui mama ntilie, kwenye eneo la mradi ambao ni wa mchina kwenye nchi Yao wenyewe.

Mm nilifikiri kuwa ludewa ndo itakua ndio sehemu sahihi. Ambapo vijana wa nchi hii watapatia mitaji na uzoefu katika sector ya viwanda Kwa kuwa ndio sehemu pekee ambapo makaa ya mawee na madini ya chuma vipo karibu. Hivyo itawarahishia vijana kuanza chini Kwa teknolojia ya kawaida na kukua na kupata teknolojia kubwa ambayo itawasaidi kwenda kuwekeza kwenye maeneo ambayo yatahitaji teknolojia na mitaji Mikubwa. Swali Sasa CCM Leo hii mnaamua kuwapa wa wachina mali tuliyopewa na mwenyezi mungu ambayo ni rahisi hata kwetu sisi kudeal nazo ila man aka kumpa mchina tena Kwa mvutano sana ambapo mchina anataka faida kuliko uwekezaji. Je na hayo maeneo mengine ambako ni kugumu mtampa mchina mta yaacha alidhini.

Mm nilifikiri wachina wamepewa fursa kwenye uwekezaji wa viwanda lakini kwenye malighafi anapewa mtanzania. Kwa maana nimeona viwanda pale makambako vinajengwa na nimeambiwa Nivya vyuma mm nilijua labda mnasogeza wawekazaji ila kule ludewa vijana wa Tz waanze kazi.


View: https://youtu.be/MRGEoW9YI6U?si=QtIAEorUKSofnfNh


CCM inatufelisha sana
 
Tatizo tuna viongozi vichaa. Makaa ya mawe yalitakiwa tuyachakate wenyewe ili kupata vipuri mbalimbali Kwa maendeleo ya Nchi yetu.Lakini viongozi wa awamu ya sita na upuuzi wao wanaofurahia makampuni ya kichina kuchimba makaa ya mawe na kuyapeleka kwao matani na matani Kwa ajili ya uchakataji na kutuzuia Tena sisi.Tunaongozwa na vichaa
 
Tatizo tuna viongozi vichaa. Makaa ya mawe yalitakiwa tuyachakate wenyewe ili kupata vipuri mbalimbali Kwa maendeleo ya Nchi yetu.Lakini viongozi wa awamu ya sita na upuuzi wao wanaofurahia makampuni ya kichina kuchimba makaa ya mawe na kuyapeleka kwao matani na matani Kwa ajili ya uchakataji na kutuzuia Tena sisi.Tunaongozwa na vichaa
Achaa mkuu nimepiga hesabu Hapa Kwa kijana kutoboa Tz katika sanyansi na tech ni ngumu china ya wanaccm
 
Back
Top Bottom