Hivi inakuaje kama ukiwa umejisajili NSSF halafu haufanyi malipo?

Hivi inakuaje kama ukiwa umejisajili NSSF halafu haufanyi malipo?

Idrissou02

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2018
Posts
354
Reaction score
656
Mimi nilijisajili NSSF mwezi May. Kulingana na taratibu za ofisi yetu bado mwajiri wangu hajaanza kutuma hiyo fedha huko. Hivi kule wananiandikia deni au inakuaje? Msaada wakuu
 
Salary Slip inasemaje? Kama haujaanza kukatwa inamaanisha haujaanza lipa.

Hauandikiwi deni boss.
 
Asante. Na ukishaanza kulipa ukipitisha mwezi bila kulipa haileti shida?
Salary Slip inasemaje? Kama haujaanza kukatwa inamaanisha haujaanza lipa.

Hauandikiwi deni boss.
 
Mimi nilijisajili nssf mwezi May. Kulingana na taratibu za ofisi yetu bado mwajiri wangu hajaanza kutuma iyo fedha huko. Hivi kule wananiandikia deni au inakuaje? Msaada wakuu
Wanakuwekea sifuri tu,hakuna deni.Siku mwajiri akipeleka wanakujazia.
 
Hivi kama boss alikuwa hapeleki na mkataba ukaisha mkaachana unafanyaje apeleke malipo yako?
 
Hivi kama boss alikuwa hapeleki na mkataba ukaisha mkaachana unafanyaje apeleke malipo yako?
Nenda ofisi za nssf zilizokaribu nawe,nenda ofisi ya malalamiko,utapewa form utaenda nayo kwa mwajiri ataijaza na watamkaba atalipa.
 
Nenda ofisi za nssf zilizokaribu nawe,nenda ofisi ya malalamiko,utapewa form utaenda nayo kwa mwajiri ataijaza na watamkaba atalipa.
Hivi kama Mimi nilikua nafanya kazi na KAZI ikaisha. Na boss wangu amefariki, na fedha yangu ipo nssf. Nafanyaje Ili niipate?? Maana Sina wakunijazia zile fomu za michango
 
Back
Top Bottom