Kasomi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 11,030
- 20,391
Maisha hayapo sawa kabisa.Hili jambo linanisikitisha sana, pamoja na watu kutumia ID fake inakuaje bado wanakuwa na wasiwasi hadi wanajivisha jinsia zisizokuwa zao?
Kidume kabisa kinatumia ID fake lakini bado kinajivisha jinsia ya kike. Kuna wakati utakuja upate tatizo na ukahitaji members wakusaidie unakuja tambulishwa ni mkaka au mdada na huku ulituaminisha wewe ni mdada au vinginevyo hakutakuwa na wa kukuamini.
Siwaingilii haki zenu lakini i find it to be strange aisee.
Mtu anaandika kike kike na kujitamburisha kama mwanamke hadi mnakula pesa zetu tunahisi tumeopoa mirupo kumbe vidume bwana.(utani) lakini haipendezi kabisa japo siwapangii maisha.
Mwanamke akijifanya mwanaume anaonekana mjanja, ila mwanaume akijifanya mwanamke anaonekana mjinga.
Waache wanasababu zao.