Elections 2010 Hivi inakuwaje unaomba kupigiwa kura kwa staili ya "kupiga magoti"?

Elections 2010 Hivi inakuwaje unaomba kupigiwa kura kwa staili ya "kupiga magoti"?

Baba_Enock

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Posts
7,076
Reaction score
2,457
Alianza Shamsa ... sasa naona Shy-Rose anafuata nyayo.... Inawezekana huna chochote cha kuwaambia wapiga kura zaidi ya kupiga magoti na kuomba wakuchague?

Jimbo la Kinondoni

Mgombea ubunge, Shy - Rose Bhanji, alipiga gwaride na kupiga magoti kuwaomba wananchi wampe nafasi hiyo huku akisisitiza kuwa kitendo chake hicho ni kuonyesha unyenyekevu na ukomavu. Mgombea mwingine Mpoki Mwambulukutu, alikuwa akitembea na vyeti vyake vya taaluma ili kuwaonyesha wananchi uwezo wake wa kielimu na kitaalamu.

Source: Imeripotiwa na : Tanzania Daima/Mwananchi/Nipashe
 
hiyo ni awamu ya kwanza, namaanisha ndani ya CCM, sasa tusubiri awamu ya pili wakipambana na wapinzani nadhani hapo watapita kila nyumba kwenda kufagia na kuosha vyombo
 
Huyu Shy Rose nimeangalia hata facebook yake kaandika kuwa kawaomba wanaume wagombea wamwachie apite yeye maana yeye mwanamke. Hivyo yeye anahisi ubunge sio ability ila ukiwa mwanamke, kijana, kilema basi. Hata UWT inabidi ability sijui anafikiri nini
 
Yaani mi nimabaki hoi...
Sikutegemea na yeye kuwemo kundi hilo..
 
KUPIGA MAGOTI SI JAMBO LA AJABU SAAANA KAMA MUNAVYO LIKUZA WANAJAMII,,
LAKINI HOFU YANGU MIMI NI UWEZO WA WANAWAKE KATIKA UONGOZI, KWASABABU WANAWAKE WANAFIKIRI SASAHIVI UKIWA MWANAMKE TU UNAPATA NAFASI YA KUGOMBEA UBUNGE FIKRA AMBAZO SI ZA KWELI.. SASA SHY NAE ANAFIKIRI ANAWEZA KUONGOZA KWASABABU YEYE NI MMOJA WA WANAWAKE AMBAO WAPO NA UMAARUFU WAO.. KUNA WANAWAKE WENYE UWEZO MKUBWA SANA WA KUONGOZA LAKINI HAWAVUMI MIKOANI NA HATA DAR PIA.:shock:
 
Mkisha wapa ndo hamuwaoni tena mpaka 5yrs wanarudi na huruma hiyo hiyo.
 
Sikujua kuna wagombea wako desparate kiwango hiki!!

desparate on what! mkuu it is all about monies.

Ukiwa mjengoni dodoma for five years mshahara, marupurupu, vikao etc ni zaidi ya tsh 500ml for five years. Hapo hujawa waziri wa Madini na Nishati ukasainishe mkataba wa kuuza nchi Guest House jijini London.
 
Sikujua kuna wagombea wako desparate kiwango hiki!!

wanafiki wakubwa hao. wameishiw ambinu za kuwadanganya watz sasa wanafanya michezo ya kitoto tu.....hiyo yote ni kutafuta njia ya kuapata ulaji.

Si wauze sera zao watushawishi tuwachague?? why would one beg that much? Hivi kweli tumekuwa wa kudanganywa kw akupewa shikamoo na kusalimiwa kwa kupigiwa magoti???
 
Hawana jipya la kueleza au hata kufikiri kwamba watalitenda..
Wanategemea huruma za wapiga kura wakaneemeke..
 
Huko mbele baada ya kuanza kampeni -- akibanwa sana na Daktari Mpiganaji, Mkuu wa Kaya anaweza naye kupiga magoti. Lakini hii itakuwa tabu kidogo kwake kwani alisha watukana wafanyakazi wa nchi hii.
 
Aje aoshe vyombo nyumbani kwangu nitamfikiria, au nitampa ajira kabisa na mshahara wa wabunge wenzake
 
As a woman I was happy kusikia mwanamke anagombea lakini alinitia aibu anavyofikiri kuwa kwasababu mwanamke basi wanaume wamuonee huruma wamuachie nafasi. Yani when I heard her begging at the campaign when she has no substance at all and cannot even debate the issues I felt foolish to have been previously excited at the thought of a woman running for the position. Recognition of our abilities is what we women fight for and not pity as she thinks.
 
Ukisikia watu wameishiwa sera ndo hivi, kama kuomba kura za kuteuliwa kugombea ndani ya chama inakuwa hivi, je akipitishwa kwenye kinyang'anyiro chenyewe itakuwaje, si ndiyo atataka arambe viatu vya wapiga kura?
 
Back
Top Bottom