hivi inawezekana ama ni kwangu tu?

Hiyo hali huwa inajitokez ndio mrembo, ila unajipa moyo tu, ni mambo ya mpito kwenye ndoa, jaribu kufikiria mazuri aliyokufanyia, coz, kati ya hayo mabaya unayoyaona kwake lazima kuna mazuri, hakuna binadamu perfect,na uspende kumfananisha mumeo na wanaume wengine kila mtu ni unique in their own way, wanaume wengine wana upendo wa kweli mioyoni mwao lakini hawana mzuka wa kuiga mambo ya kizungu ya kufunguliana milango na mengineyo....but usiwe na wasiwasi itapita wewe ni binadamu na hiyo ni hali ya kawaida
 

Nakuhakikishia kuwa hizo ni sifa za shetani tu na si vinginevyo!Kavuruga amani wiki nzima nyumbani kwako halafu kakukutanisha na huyo mbaba ili uchanganyikiwe na uisaliti ndoa yako.
Chonde chonde, hangaikia ndoa yako, delete uyo mwanaume kwenye kichwa yako mapemaa ili umshinde shetani na pindi mawazo yako yakielekea kwake kemea!
 
Ulichonacho ni cha thamani zaidi kuliko huyo uliyekutana naye kwenye gari.Shika sana ulichonacho.
Vunja ukimya sema na mume wako.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Ukweli Ni Kwamba' Usimjaji Mtu Kwa Jinsi Anavyoonekana Au Anavyokutendea Kwa Siku Moja Tu. Kumfaham Mtu Vizuri Inachukua Time Sana May Be Utakapokuwa Naye Karibu Mara Nyingi Zaidi. Mume Wako Ni Mtu Wa Muhimu Sana Coz Una Noleji Kubwa Juu Yake, Unafahamu Mapungufu Na Mazuri Yake Hivyo Una Uwezo Mkubwa Wa Kuyabalansi Kwa Kadiri Iwezekanavyo. So Deal With Your Husband Pliz! Tunapendezwa na wengi sana barabarani, je hao wote ndo tuwe nao? tutakuwa na wangapi? Hebu Jiulize Umeshapendezwa Na Wangapi Katika Maisha Yako. HAYA BWANA!!!
 
Maumivu ya kichwa huanza pole poleeeeeeee
 
nina miaka 35, kuoa sijaoa ila sasa sina ujanja itabidi nioe kukamilisha ratiba, sababu ni uwezo wa kufikiri wa nyie wapendwa wetu, mfanyie mwanamke mema mengi muudhi mara moja atokee mtu amfurahishe mara moja huyo wa mara moja atapeta. ndio maana kwa muda wote nilikuwa opputunist nikiutumia udhaifu na nilifanikiwa ila haramu itabaki kuwa haramu na halali itabaki kuwa halali.
 
Hakuna mkamilifu! Una muona ana kujali sababu ajakuweka ndani! Najua hata kabla hauja olewa mmewako uliona ana kujali sana! Usiache mbachao kwa::::::::::::::::::::::::::::::::

na hapa wanawake wengi ndipo huwa sehemu ya kuwapata, akisha umizwa tu, yan ana kuwa mwepesi ningekuwa huyo mzee ninge akikisha unaingia kwenye mtego alaf baadae na kuongoza toba.
 

kaka nakushukuru na pia samahani kwa kuwa mbaali na mtandao na naomba nikujibu ifuatavyo:-
-siyajui mema wala mabaya ya huyu bwana but ya mr nayajua vizuri tu
-kama mwanaume wapo wengi tu waliovutika kwake ama aliovutiwa nao
-nitakaa pembeni
-huwez kulinganisha manake ya mume imezid
-naye sipendi afanye hivyo

mkuu ngoja nikwambie kitu kama umeisoma vizuri post yangu ni metamatisha kwa kusema siyo kwamba simpendi mume wangu, na pia nimebainisha mambo ambayo mimi kama mwanamke yanaweza kunikuta na kusababisha niingie dhambini.

kaka sikuolewa staili ambayo tuichukua gest ama disco, na katika wanawake wavumulivu naweza kusema miye nami nimo na pia wanaojali familia ila nimeamini kweli kua penye miti hapana wajenzi. na kweli Mungu hakupi vyote.
 

niwie radhi kwa kuchelewa kukujibu, mkuu miye naweza kujiita mwanaamke na mke bora, sijisifu bali hata ndugu na marafiki wananisifu kwa hilo. Tatizo ni kwamba mwenzangu naona pesa zinamchanganya sana kiasi kwamba anathamni marafiki kuliko mimi.

mume wangu hajui hata mara ya mwisho alinunua leso lini, wala hajui hata kujifunika kitandani ni kazi yangu kuamka na kumfunika kila siku, kaka sijui dada nafanya kazi kwenye shirika la kimataifa maisha yangu kiuwezo ni mazuri sana kiasi kwamba mume hajawah kusumbuka kuombwa hela wala nini na nawajali wakwe zangu kuliko mwanamke yeyote ila jamani mume wangu na pombe na marafiki na hivi anavijisenti nakoma.
 

kaka Mr Rocky naomba nikujuze kitu fulani hivi manake post yako hii imenifanya niseme hata nisiyotaka kuyasema.

Mimi na mr tumeoana 5 yrs back by then nilikuwa na miaka 27 nilikuwa najiendeleza kielimu ngazi ya masters na ni mfanyakazi kwenye moja ya mashirika ya UN. mpaka hapo nilikwa ni binti ambaye ni virgin na huwez kuamini niliolewa na mwanaume mwenye mtoto tayari. na nilimpenda huyu binti kiasi cha yeye kuamua kuishi na mimi kama mama yake na mpaka leo naish nae. Mimi ni mwanamke wa kikristo ambaye nilisha sema sitokaa nivue nguo yangu kwa mwanaume zaid ya mmoja maishani mwangu na mpaka leo hii sijawah wala sitarajii. u can have an idea ya wanaume ambao nakutana nao ama wanaonitongoza ni wengi sana tena wenye pesa but kwangu miye hilo huwa siafiki kwani si kwamba nalinda heshima ya mume la hasha ila natunza heshima ya mwili wangu and thats all.

nilalamikapo juu ya care za mume wangu kaka nimejitahd sana, sijawah hata siku moja kutotimiza wajibu kwa familia yangu, lakini sioni mwenzangu akifanya hivyo. nafikir kwa jinsi alivyo na mihela mingi basi yeye kaamua marafiki na pombe ni bora kuliko miye mkewe. nimeshasema na kulia sana na kusali sana sasa nimefika mwisho nasubiria neema ya mungu tu ila ukweli ni kwamba wanaume mnashawish wake zenu kutoka nje ya ndoa.
 
Last edited by a moderator:

dada nakushukuru sana, kwakua hujaolewa siwez sema sana lakin utakapoolewa utajua kwanini nimewaza hivi. Binafsi kwa status yangu siyo mtu wa kutembea na wanaume hovyo hovyo kwani ni mke wamtu na mama na pia najipenda sana na hasa napenda kutunza heshima ya mwili wangu.

lakini jamani wanaume wanakosea sana wanapoacha kututhamini.....................jamani naomba nisiseme sana manake nalia kwa uchungu naamani siku nkulete kwangu uone hali ilivyo
 
Kwa maelezo ya kisa chako ninashawishika kwa aslimia 100 wewe ndio tatizo kwenye ndoa yako na si mumeo kwa maneno machache inaonekana HUJATULIA unahitaji KUPEPEWA.Unachokitafuta utakipata tu.

ndugu yangu TUMY sidhani kama kwa kalamu yangu waweza nihukumu, lakin sasa naamin kuwa asiyekujua hakuthamini. so ni sawa tu
 
Last edited by a moderator:

ndugu wala usishangae maneno yangu ama sentensi hiyo imeficha mengi sana ndani yake ambayo siwez kuyasema. hivi unafikir mume wangu hana mazuri anayoyafanya? ama wadahni nina underestimate mapungufu ya kibinadamu? la hasha najua fika kuwa hata hawa wanaotongoza ni hao hao but inaumiza sana pale unapojitoa kisha mwenzi wako haitoi aisee
 

manshiroo asante sana kwa ufafanuzi wako na nimekupata
Ila naomba kabla hujaamua kutoka nje au kuupokea wema wa huyo baba aliyekuja kwako jiulize maswali mengi sana kichwani mwako. Kama uliweza kuapa kuwa hutomvulia mwanaume yeyote nguo zaidi ya mumeo nenda na kiapo chako na wala usikiache
Nilalokuambia usidanganyike huwezi jua huyo jamaa anataka nini kwako au ana matatizo gani kiasi cha kuamua kukufanyia hayo
Anaweza kwa vigezo vyako akawa mwanaume wa kukucare sana na kukupenda upendo wa dhati ila vile vile anaweza kuwa nyoka ndani ya ngozi yake
Jiulize na jihoji mara mia mia kabla ya kukuba,li kuanguka na kuusaliti utu wako
Na jingine hebu siku moja jifunge umuombe outing mumeo mwende nae mbali na hizi kelele za magari na watu mkae mahali upasuke kila lililo moyoni mwako na mweleze kwa utaratibu kuwa hili na hili haliko sawa na jishushe mwambie kama na wewe kuna sehem uko wrong anzeni upya kama wakati wa uchumba
Ikiwork out you have your husband kama sio hapo sitakuwa na la kukushauri tena
 
Last edited by a moderator:

ahsante sana kwa ushauri mzuri najua siwez kutoka na huyu mtu nisiyemjua na ambaye si mume wangu kamwe kwani maisha hayapo kwenye kucare tu yapo pia katika sehem nyingine. ila hapo kwenye red mbona kama umenawa mikono mkuu? so inamaana hata humu jf nisitegemee mawazo ya kunijenga tena?
 

Nimetoa ushauri wangu kwa kweli manshiroo na naomba uuzingatie
Nipo kwa wakati wote na wengine wapo watakupa ushauri zaidi na zaidi hatutachoka
 
Last edited by a moderator:
itakuwaje uchanganyikiwe na mapenzi ya siku moja?unahuakika gani kama anamfanyia hivyo mkewe au mpenzi wake?mpende mumeo hayo ni mapungufu aliyonayo yaweke sawa..

MWANAMKE MPUMBAVU UIBOMOA NYUMBA YAKE KWA MIKONO YAKE MWENYEWE..
 
ndugu yangu TUMY sidhani kama kwa kalamu yangu waweza nihukumu, lakin sasa naamin kuwa asiyekujua hakuthamini. so ni sawa tu

Ndugu yangu Manshiroo. inawezekana usemi wako kwamba asiye kujua hakuthamini ukawa ni sahihi in some circumstances ila kwa ishu yako naendelea kusimama kwenye kile nilichokisema kwa kuwa umeonyesha udhaifu wa kupitiliza na kwa maneno mengine wewe pia si mwaminifu, sina lengo la kumtetea mumeo ila kaa ukijua kwenye ndoa kuna ups and down sasa kama wewe tatizo kidogo tayari umeshaanza kuonyesha ufa kiasi cha kukiri wazi unaelekea kutaka kuanguka dhambini huoni kama hilo ni tatizo, sasa huyo umekutana nae siku moja ungekuwa na unakaa huko wiki nzima sio ndio ungesahau na nyumba yako kabisa, kaa chini na mumeo mumalize matatizo yenu huko unakoona wewe ni salama usikute wenzako nao wanatafuta watatokaje.
Hivi kama wewe ni mtu mzima na una akili timamu kabisa unataka kuniambia hujui what is behind that man,use ur common sense utaruka ruka hivyo mpaka lini, angalia kuna magonjwa ndugu yangu lakini pia kumbuka mwanamke mjinga ataivunja nyumba yake yeye mwenyewe vivyo vivyo kwa mwanaume.
Pamoja na kwamba hatujui una miaka mingapi kwenye ndoa yako, ila hata kama mumeo ana matatizo text yako imetoa picha ya wewe ni mtu wa aina gani na kweli unahitaji ushauri tena serious ama kama si hivyo kuna mengi yako nyuma ya pazia labda.
My take:Tulia jenga ndoa yako wacha hayo mawazo ya kuruka ruka hayatakufikisha popote.
Bye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…