Hivi inawezekana mapenzi ya dhati kuibuka kwenye mawasiliano ya simu?

Hivi inawezekana mapenzi ya dhati kuibuka kwenye mawasiliano ya simu?

Papa Mopao

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2009
Posts
4,153
Reaction score
2,647
Hii imenitokea mimi hivi punde!!

Stori ni hivi:

Unajua kuna siku wakati nafanya kazi ya Customer care ofisini, nilipigiwa simu na mteja akanieleza tatizo lake na baadaye nikamtatulia tatizo lake, sasa baada ya muda mfupi akanipigia tena juu ya huduma nyingine zinazohusina na huduma ya ofisi.

Hapo sasa ndo ilikuwa mwanzo wa mahusiano yetu, unajua ilikuwaje? Badala ya kuzungumzia khs huduma akazungumzia vitu vingine nje ya huduma za ofisi, mambo aliyoyagusia ni kama ninaishi peke yangu, au nina mchumba na mengine mengi.

Lkn kinachonishangaza kila akipiga simu topic ni nyingine na si ya kujirudia! Kwa muendelezo huo umetufanya tuwe karibu sana kimawasiliano na mpaka tukafikia hatua ya kujiuliza kwanini imekuwa hivyo? Huyu kwa kweli amenipa wakati mgumu sana.

Hivi inakuwaje kuwaje kufikia kiasi cha kuzimiana kwa mtindo huu? Mimi huwa najiuliza sana khs hili maana haijawahi kunitokea asilani, nikahisi labda alivyoniuliza kama nina mchumba nikamjibu sina,nikahisi labda hilo ndo sababu!!!
 
Unafanya customer care siyo?
Hivi ofisi yenu haina utaratibu wa kurekodi maongezi ya wafanyakazi wao na wateja in case of anything?
Huyo mtu wewe ndiye umempenda au yeye ndo kakupenda?
Je, kwenye hiyo ofisi ni wewe tu unayefanya hiyo kazi ya customer care?
Je huyo mtu huwa anakueleza khs maisha yake au ni wewe tu unayeelezea ya kwako?
Angalia isije kuwa unachorwa halafu unajiingiza kichwa kichwa ndugu...

Otherwise: Good lucky, Anything can happen...
 
inabidi uwe makini kidogo papa japo mapenzi mengine yanaanzaga kiajabu ajabu lkn hapo kuwa makini kaka yangu.
 
Unafanya customer care siyo?

Yap!
Hivi ofisi yenu haina utaratibu wa kurekodi maongezi ya wafanyakazi wao na wateja in case of anything?

Inao huo utaratibu!

Huyo mtu wewe ndiye umempenda au yeye ndo kakupenda?

Kwa mara ya kwanza alinipigia simu topic ilikuwa inahusu tatizo analotaka atatuliwe nikamsaidia, sasa alipiga mara ya pili yeye mwenyewe...

Je, kwenye hiyo ofisi ni wewe tu unayefanya hiyo kazi ya customer care?

Tupo wengi sana...

Je huyo mtu huwa anakueleza khs maisha yake au ni wewe tu unayeelezea ya kwako?

Yah nilipoona ananiuliza khs nina mchumba na mambo mengine imenilazimu nimchokoze kwa kumuuliza maswali yanahusu maisha yake...

Angalia isije kuwa unachorwa halafu unajiingiza kichwa kichwa ndugu...

Shukrani mkuu kwa tahadhari!

Otherwise: Good lucky, Anything can happen...[/QUOTE]

Inawezekana...
 
mmh sasa apo unashangaa nin?mshapendana labda tak nxt step msome na yeye ujue km yupo poa that hana mtu +ana nia ya kweli nawewe isije ikawa ametumwa kukufatilia then wewe unavmbisha bichwa tu ...
km vp ol da best....asi hauna mchumba bas mfanye mchumba uyo au?ushamwona lakin kwa macho?isije ikawa ni bimkubwa fulan ivi ,au MFANYABIASHARA.....
 
Rose kwanini unasema hivyo??
ahh babuweee kwan aujui?
yes anaweza akawa ni mshugamami mmoja ivi anayetafuta damu mbch....au ni m.a.l.a.y.................anayetafuta wateja kwa njia ya cm bt stll anaweza KUWA NI MDADA TU DECENT AMEKUDONDOKEA anythng can b............!!!!!!!
mshawai kuonana kwanza......?????
 
hehehehehe pole sana na nyie bwana namba zileeeeeeeeeeee za customer care mnatumia kwa mambo mengine ..
 
Uwe makini mchunguze huyo asije kuwa hana mapenzi ya kweli. Katika maisha lolote lile linawezekana na mambo haya huwa yanaweza kukutokea kwa njia yoyote mkaanzisha mahusiano na kuoana kabisa. Swala la muhimu usikimbilie kuoana na mtu ambaye humjiui vizuri mchunguze kwanza. Otherwise hakuna noma.
 
Back
Top Bottom