MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Hapa nawaza na kuwasilisha, mahakama ya Kenya imebatilisha matokeo ya uchaguzi kwa kile ilichokitaja kuwa ukiukwaji wa katiba na tume huru ya uchaguzi. Japo mahakama iliomba muda ili itoe maelezo kamili kuhusu ilivyofikia kwenye hayo maaamuzi, hivyo kwa kifupi hadi hapo hakuna anayejua nini sababu haswa za kufutwa kwa matokeo, sote tunasubiri kwa hamu taarifa kamili.
Ninachojiuliza, hivi inawezekana tukarudia uchaguzi na ufanyike mwanzo hadi mwisho bila dosari? Ama ndio tena tutajikuta kwenye hali hii hii baada ya siku sitini zijazo. Kama Wakenya tumejiandaa vipi, maana kampeni zimeanza, hivyo inamaana tutaburuzana kwa miezi miwili ijayo, ikumbukwe pia Raila naye ameanzisha mtiti dhidi ya tume, hivyo lazima patachimbika hadi awatolee nje viongozi wa tume kama alivyofanya kwa wale wa awali.
Vipi katiba inasema nini, ama inawezekana tukarudia chaguzi mpaka basi, maana kila ikitokea dosari tutarudi hapa. Binafsi nina furaha kwa kuona mahakama zetu zimedhihirisha kuwa huru, lakini nahisi sisi wenyewe hatupo tayari kwa demokrasia ya kiwango hicho.