PostGE2025 Hivi internet ikizimwa tena siku za usoni, umejipangaje?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Sasa hivi Internet ikizimwa serikali inajikwamisha pia na watumishi wake wanashindwa kufanya kazi. Everybody is affected.
Kwani hilo hawakujua? Wanajua sana hilo ila tatizo ya ubinafsi ndio hilo. Wanatanguliza maslahi yao ili kumfurahisha boss wao bila kuangalia watu wanaathirikaje.
 
StarLink zitaongezeka sana
Na pia wengi watajikita kwenye satellite zingine za dish
 
Ilikuwaje hadi taasisi kubwa nazo zilikosa Internet ilihali wao kwenye maeneo yao huwa wanafunga ma-dish maalumu tofauti na raia tunavyoifikia Internet. Je, yale ma-dish huwa yanakamata mawimbi ya Internet kutokea wapi hadi wakumbwe na blackouts ambazo huwa. zinawalenga raia?.
 
StarLink zitaongezeka sana
Na pia wengi watajikita kwenye satellite zingine za dish
Hizi labda ziwe za kimagendo ndio zitasaidia, ila zikija kihalali ni lazima zifuate maagizo ya serikali.
 
Elimu nzuri, asante!
 
Starlink ndio kila kitu, Lakini kwa jinsi inavyo fanya kazi sidhani kama wanaweza kukubaliana na kufika muafaka na serekali.
Starlink hawana kona na wala haihitajiki ofisi yao iwepo Tz ili ifanye kazi.
Kwa hili sidhani kama wana weza pewa ithibati.
 
Kuna watu waliweza kupandisha contents humu. Server za JF zikipata wapi Internet?.
Kuna wengine walikuwa nje, of course wao hawakuathirika na shut down, so waliweza pandisha contents, lkn pia kama unatumia huduma kama hizo obvious waliweze ku-navigate! Pascal Mayalla najua wewe ulikuwa una access ya net naomba uzoefu wako mwenzetu ulipataje au hukuwa nchini usikute ulikuwa kwa kina Mark au Linda hahaa (joking)...
 
Me nilikuwa hapahapa nchini, yes kuna members wapo nje, ila ilikuwaje Server za JF ziliendelea kufanya kazi ya kupokea contents ilihali Internet ilizimwa?.
 
Ahahahahaha michoro ujaacha tuu we jamaaa...

Sema kwa siku naingiza 5000 mkuu huwa natamani kulia ujue daaah acha kabisa...

Sijui nitafute kazi serikalini tuuu 🤣🤣🤣🤣🤣
Vipo hawakuchoma kakibanda kako mkuu, kama walichoma basi watakua walisaidia maana kalichoka mno mkuu.
Jenga tu kengine na zile spika pia badili.
Mishangazi inakupa pesa, wewe unatoa kwa vitoto vya afu mbili.
 
Vipo hawakuchoma kakibanda kako mkuu, kama walichoma basi watakua walisaidia maana kalichoka mno mkuu.
Jenga tu kengine na zile spika pia badili.
Mishangazi inakupa pesa, wewe unatoa kwa vitoto vya afu mbili.
Wamebeba na WiFi yangu mbwa hawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…