Michael Amon
JF-Expert Member
- Dec 22, 2008
- 8,768
- 3,622
Kwa kweli hawa BRELA wameniudhi sana kwa kutokuwa makini katika kusajili majina ya biashara. Mnamo tarehe 6 december mwaka jana nilienda katika ofisi zao ili kusajili jina langu la biashara na mara baada ya kusajili nililipia malipo na kupewa risiti na kuambiwa nije nifuatilie certificate of registration.
Kutokana na shughuli nyingi na kuzungusha pale katika ofisi zao kuwa certificate of registration bado haijakamilika niliamua kurudi zangu nyumbani na kumwachia ndugu yangu mmoja anisaidie kufuatilia hizo certificate of registration.
Siku si nyingi huyo ndugu yangu alifanikiwa kuzipata hizo certificate of registration na juzi ndio amenitumia.
Lakini cha kushangaza baada ya kupokea certificate hizo jina la biashara lililoandikwa hapo ni tofauti na lile nililolisajili. Hivi jamani kweli huu ni uungwana? Mnashindwa kuwa makini hata katika vitu vya msingi kama hivi?
Siku nikienda dar nitaenda kupambana nao na lazima watanirekebishia tu.