Hivi JamiiForums kuna watu bado hamjawahi kushika hata milioni moja?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Mimi naamini humu ndani wote tumewahi kukutana na vibunda kwenye ma deal yetu makubwa yaani namaanisha mzigo wa maana milioni kwenda mbele kwa mara moja paap.

Maana humu Wengi Ni wafanyakazi Wenye mishahara minene na wengine ni wafanyabiashara wa Kati na na Tena Wengi tumesoma Soma Chuo Kikuu tuna laptop za gharama au iPhone na Wengi tu Wana magari.

Siamini Kama Kuna member fukara kabisa ambaye anakosa hata laki tatu ya haraka haraka Hapo alipo.sasa Nina ishu nataka niwashirikishe wale ambao mpo serious tuanzishe group maalumu na Tena maxence melo awe ndo mweka hazina wetu kila week tunachanga 7000 baada ya mwaka tutakuwa na hela nyingi Sana kisha tunaenda kwenye soko la hisa au tunafungua fixed account tunawekeza pale hela yetu baada ya miaka mitano tutachukua hela yetu tunagawana.tuko Wengi wenye uwezo naamini hata billion 1 tukichanga zinafika.

Imagine ukachangia kila week 7000 baada ya mwaka utakuwa umechangia zaidi ya million tatu haya assume members kwenye Hilo kikundi tuko 10000 jumla itakuwa billion 30 haya tukapeleka fixed account baada ya miaka mitano interest ikazaa billion 50 haya wengine wakafa hata members 3000 tukabakia 7000 tukija kugawana hip hela kila mtu anaondoka na milioni Zaidi ya 100
 
Hata mimi siamini kwanza tangu ni join Jf napata mbinu nyingi humu nimeongeza productivity yangu maradufu
 
Vipi boss, unataka kutugawia au unauliza tu kujifurahisha??
 
Kuna mfanyakazi mwingine wa kada yako amemuua mwenzie kisa kaambiwa "una roho mbaya kama sura yako, ndio maana kelvin hakuoi"
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]lol
 
Nijibu kutokana na heading,tupo ambao hata laki tu kushika ni shughuli[emoji27]
Umeanza chai zako


Lile gari lako vipi tayari ulishampata mteja wa kulinunua ?? [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Umeanza chai zako


Lile gari lako vipi tayari ulishampata mteja wa kulinunua ?? [emoji3][emoji3][emoji3]
Jf is a dampo walahi.ukisikia stori zetu unaeza ukadhani tunafanya miamala ya mamilioni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…