Hivi jengo la Spika lenye thamani ya Tshs. milioni 500 lililojengwa Urambo nani analitumia sasa?

Hivi jengo la Spika lenye thamani ya Tshs. milioni 500 lililojengwa Urambo nani analitumia sasa?

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
11,795
Reaction score
36,704
Nakumbuka Sitta aliipata mwaka 2010 kutoka kwa Slaa kutokana na ujenzi wa hili jengo.

Aidha, nakumbuka siku Kikwete analizindua alipokuwa Rais aliguna kisha akasema "Sasa kila mtu akijijengea hivi kutakalika kweli"

Nani analitumia sasa? Maana ni jengo la hadhi ya Spika lililojengwa kwa kodi zetu Tshs milioni 500! Slaa alipiga kelele sana, natamani nimsikie kwenye uwanja wa Chato na daraja la Kigongo Busisi ambavyo ni machaka y ufisadi ya John Magufuli.

Marehemu Sitta naye alijipambanua kuwa ni mzalendo kama alivyo John Magufuli, tofauti yao ni kuwa mmoja ni dikteta huku mwingine aliruhusu uhuru kwenye mhimili aliokuwa anaongoza!

Ila wote wanajisifu kwa uzalendo na kupinga ufisadi!
 
Serikali ina shughuli nyingi zinazohitaji majengo,inaweza hata kuwa mahakama
 
Back
Top Bottom