Nashukuru ndugu zanguni kwa mada hii inaonekana ya kitoto lakini ukweli mtaujua baada ya maelezo haya hapa chini
1- Joti ni msanii, na mara nyingi msanii anaigiza mazingira ya watu wa jamii yake au karibu na jamii yake,mfano afrika muvi nyingi zinaongelea mambo ya kishirikina kwani ushirikina umetawala sana africa. Sasa kama mtu anaigiza kitu ambacho hakipo anakifanya kizoeleke ktk jamii husika inayoona kitu hiki.Mfano Zamani kulikuwa hamna tv za kuonesha miziki y magharibi sana(rap,hip hop etc ndio maana watu walijikita kupenda nyimbo za zipompapompa na za kina chidumule,lakini punde tv,video zilipo kuja kwa kasi watu ndo wakaanza kiuwajua kina Mc Hammer,tupac etc. Hapa joti anauingiza ushoga taratibu katka kizazi chetu huku watu wakichekelea,
2- Kwa hapo juu kuna mtu anasema kuna wengine wanaigiza ujambazi na kutumia silaha, hata kama huyu mtu si jambazi mtoto wako au wa jirani yako atajifunza kwamba kuua ni kawaida kupitia msanii huyu kama tunavyoona marekani mtoto alipoamua kutekeza mwalimu na wanafunzi wenzake.
3- Joti anapanda mbegu ya ushoga ambapo wewe bado kuona matunda yake kupitia mwanao ambaye hajakuwa tuu na hii roho kutenda kazi ndani mwake.
Angalizo: Huyu joti,movie za ujambazi,na tamthilia kwako wewe unaweza kuweka limit kwani akili yako imekomaa lakini kwa kizazi kidogo au mtu mzima ambaye hajakomaa fikra inakuwa ni hatari ( Kuwa mwangalifu)