Hivi kama baba kaikimbia nyumba, nini hatma ya kijana mwenye ndoto?

Acha ateseke tu hiyo ni karma ujinga alioufanya 2015 na watu wake wa IT ndio unawatafuna hakuna huruma
 
Kwa vile haijawa rasmi Ngoja tuendelee kufuatilia kwa majirani Maana wao wenyewe Hawajajitangaza. Ila story za Majirani tuendelee kuzifuatilia by the way hao wazazi wawili watarudishwa na wale babu zao watatu waliobakia yule babu wa kusini yule babu wa Pwani na Na yule Babu Mzaa mama ambaye ukitaka kwenda kwake kwa miguu huwezi labda lazima ubwebwe ndio ufike kwake. na njia zake ni mbili tuu juu na kuchezea Mmaaaaa.
 
Alishapotezwa siku nyingi,majuzi alikuwa akilia lia katika kikao cha Dr Bashiru.
 
Mbona ndilo eneo la kujigamba kwake hivi sasa? Pia kawaleta mashushu kibao wakijifanya makahaba, kumbe anatupeleleza. Sijui anatupeleleza kwa nyanya zipi!

Juzi kati mmoja wa hao mashushu wake kanifuata hadi ofisini... Alificha Ila baadaye alikubali...
Khah; kwa wanavooperate Ni wazi Tumekuwa watupu sana!
 
Hao mababu kuna dalili watapuuzwa aidha na wenye makali au wakimbiaji mwenyewe.
 
Kijana kwa kuwa hakuwa mkorofi kwa familia za majirani, anaweza kwenda kujisitiri katika mojawapo wa familia ilikuwa bora na maadili mema kwa vijana. Kwa huko atajifunza maisha na changamoto mpya, pengine itakuwa rahisi kufikia malengo yake.

Kumbuka kuwa naye pia ni mmjawapo wa wadau wakubwa ambao wana siri kubwa juu ya "bao la mkono" na hata kiongozi wa sasa wa familia kusimikwa kwa hila ktk uongozi wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alishaleta ujanja kwa kutaka kumuunga babaye, akajeruhiwa vibaya sana. Naamini hatorudia kosa.
Baba yake hatoi Matumizi Kasulu, Wilayani Kigoma. Aliacha uzao alipokuwa DC Kasulu. Naanza na hilo, ni mmoja wa Waharibifu wa Watoto alimpiga Mimba Mwanafunzi akiwa Darasa la 5
 
Mimi nadhani hatodhubutu kuomba hifadhi familia jirani ikizingatiwa anayajua yaliyompata babu kipindi kile 2015. Anaijua pia familia yao isivyopenda kutoa uongozi wa familia kwa familia nyingine.
 
Baba yake hatoi Matumizi Kasulu, Wilayani Kigoma. Aliacha uzao alipokuwa DC Kasulu. Naanza na hilo, ni mmoja wa Waharibifu wa Watoto alimpiga Mimba Mwanafunzi akiwa Darasa la 5
Embu tujikite kwenye mada. Sasa kwa kijaba itakuwaje miaka ijayo?
 
bado nina mashaka kwa akina baba hao kuacha familia , ni werevu na wamelea familia vizuri kwa miaka mingi japo kunamapungufu ambacho ni kitu cha kawaida kwenye familia, nadhani kuna ajenda kubwa wanafamilia wamekubaliana sisi hatujui kiasi cha kumfanya mtoto atulie kwa kuwa analijua litendwalo na halita mzuru pengine litamjenga zaidi, rejea hawa kina baba wanaielewa familia vizuri na wanaipenda
 
Embu tusubiri, muda utaongea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…