Hivi kama nchi suala la vitambulisho vya taifa limetushinda?

Hivi kama nchi suala la vitambulisho vya taifa limetushinda?

Exile

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2021
Posts
1,477
Reaction score
3,642
Katika kero ukiachana na tanesco basi hi hawa Nida, asilima kubwa wananchi hawana vitambulisho wala namba

Na sijajua mkurugenzi wa nida ni nani na sijawahi sikia katumbuliwa au kutenguliwa hii ni changamoto sana mimi nimejaribu mara kadhaa tangu mwaka jana lakini sijafanikiwa na jana saa 11 asubuhi hadi saa 12 jioni nimepanga foleni sijajiandikisha leo nimewahi saa kumi asubuhi nakutana na foleni imenibidi nitoke tu nikatafute ugali.

Changaomoto iliyopo ni wahudumu wachache kuliko wananchi sasa serikali inatwambia kila mtu awe na nida na asitumie laini yenye taarifa za mtu mwingine je hili suala nani ataliweza?
 
Ongeza na ananwi za makazi.

Nape anakula raha tu ila kwenye uzinduzi alijisifia sana. hadi sasa yuko ofcn anakula hela ya umma.
 
Katika kero ukiachana na tanesco basi hi hawa Nida, asilima kubwa wananchi hawana vitambulisho wala namba

Na sijajua mkurugenzi wa nida ni nani na sijawahi sikia katumbuliwa au kutenguliwa hii ni changamoto sana mimi nimejaribu mara kadhaa tangu mwaka jana lakini sijafanikiwa na jana saa 11 asubuhi hadi saa 12 jioni nimepanga foleni sijajiandikisha leo nimewahi saa kumi asubuhi nakutana na foleni imenibidi nitoke tu nikatafute ugali.

Changaomoto iliyopo ni wahudumu wachache kuliko wananchi sasa serikali inatwambia kila mtu awe na nida na asitumie laini yenye taarifa za mtu mwingine je hili suala nani ataliweza
Nadhani ni vema tunapoongea tuwe na facts vinginevyo hoja zetu zitaonekana hazina mashiko. Hivi ni kweli asilimia kubwa kati ya wananchi waliosajiliwa hawana vitambulisho, kweli? Hivi ni sahihi kwamba wananchi wengi waliosajiliwa hawana namba,kweli? hii si kweli kabisa. Wananchi wengi sana wana namba za Utambulisho. Zaidi ya asilimia 85 ya wananchi waliojitokeza na kusajiliwa wana namba. Takwimu za hivi karibuni mara baada ya NIDA kuanza utaratibu wa uzalishaji vitambulisho kwa wing na ugawaji vitambulisho wa umma wamzalisha na kusambaza vitambulisho milioni 18.4 maana yake ni kwamba wananchi alimia 88.7 kati ya walisajiliwa na kupewa namba tayari wana vitambulisho vya Taifa.

Tembelea au uliza mikoa ya Mara, Kigoma, Kagera, Mtwara na Lindi wananchi wengi sana sasa takribani 95% wamepewa vitambulisho vyao. Hivi tunavyoongea ugawaji wa Vitambulisho wa Umma na kwa wingi unaendelea mikoa ya Arusha , Mbeya na Morogoro huku mikoa ya Kilimanjaro, Ruvuma, Dodoma, na Dar es salaam ikiendelea kupokea vitambulisho kwa ajili ya wnanchi wao na ndani ya wikimbili zijazo wao pia wataanza ugawaji wa Vitambulisho. Kuna kazi kubwa sana inafanywa na NIDA hivi sasa, hivyo si busara kulaumu tu kwa mazoea bila kufanya utafiti katika wakati wa sasa.

Ni kweli siku za nyuma kulikuwa na matatizo katika upataikanaji wa vitambulisho lakini ni vema tuwe wakweli kwamba hivi sasa NIDA chini ya Mkurugenzi wake mpya wnafanya kazi kubwa sana ya kuzalisha, kusambaza vitambulisho kwa wananchi kiasi kwamba kuna dalili zote kuwa tatizo hili linakwenda kuwa historia muda si mrefu.
 
Back
Top Bottom