Kutokana na mafanikio ya kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastic tumeshuhudia uzalishaji wa mifuko ya karatasi kama sehemu ya mbadala wa vibebeo.
Lakini nionavyo mimi, karatasi aina zote zinaweza kuwa "recycled" kama zilivyo chupa za plastic ili kupunguza gharama za uzalishaji badala ya kutupwa tu.
Sasa nauliza hivi tuna mfumo wa ku recycle karatasi zote kuanzia magazeti, majarida, vitabu na madaftari chakavu n.k ili kiwe chanzo cha mapato kwa wajasiliamali wadogo?
Lakini nilikuwa nasoma kwenye internet kuhusu hii mada nikagundua ku recycle karatasi kuna punguza kwa 60% gharama za kuzalisha karatasi mpya kutoka kwenye mali ghafi.HAINA FAIDA KWA SABABU ZIFUATAZO.
1.KARATASI ZILIZOTUMIKA NI RAHISI KUZITEKETEZA KWA KUZICHOMA MOTO TOFAUTI NA PLASTICS AMBAZO HAZICHOMEKI ZIKAISHA.
2.KARATASI HUTENGENEZWA KWA KUTUMIA MITI NA MITI HAIJAHADIMIKA MISITU IMEJAZANA HAIWEZI KUISHA LEO WALA KESHO.