Captain Donor
Member
- Jul 24, 2022
- 13
- 19
Kombe la dunia 2022 nchini Qatar lipo njiani.
Zikiwa zimebaki siku 47 tu kipenga cha kwanza kupulizwa wachezaji wenye timu zao zilizofuzu kushindania kombe hilo kuanza kupimana nguvu. Ni mtanange wa kusakata kabumbu! na nani mkali zaidi na mwenye bahati zaidi itajulikana siku kipenga cha mwisho kwenye fainali kitakapopulizwa mara tatu.
Ni burudani yenye kila la kustaajabisha khaswa pale ambapo wenyeji wa kombe hilo wanapokuwa wabunifu wa kutaka kuhakikisha wanafanya kitu cha tofauti na mashindano mengine yote yaliyokwisha fanyika huko nyuma.
Qatar kama nchi imejiandaa vya kutosha kuhakikisha Kombe la dunia linafanyika na kumalizika salama salimini kwa kushirikiana na FIFA lakini pia FIFA wanastahili pongezi za kutosha kwa kukubali kusogeza siku mbele kutokea Juni mpaka Novemba kutokana na hali ya hewa ya joto iliyopo kwenye nchi za kiarabu.
Mwezi Novemba ni wakati wa Masika nchini Qatar na joto huwa linashuka mpaka nyuzi joto 20, kwahiyo itakuwa ni wakati mzuri kwa wachezaji pamoja na mashabiki ambao wanapanga kwenda kishuhudia mashindano hayo.
Binafsi yangu natumai mpaka kufikia wakati huo nitakuwa mzima wa afya ili niweze kushuhudia mashindano hayo nyumbani katika hali ya utulivu na amani.