Mnafiki kwasababu ndani ya mnafiki kuna uongo na umbea juu. Mtu muongo anaweza danganya kwasababu zake binafsi na sio kwaajiri ya kukudhuru mfano unalazimisha kujua maisha ya mtu anakudanganya kuwa yeye yupo vema na ana mali ila si kweli huo uongo ni kwaajiri ya kukutoa wenge usimfuatilie mambo yake, nje ya hapo ni mtu poa sana.
Mbea anapenda kushare taarifa za watu na anaweza kushare na watu sahihi taarifa zake na isiwe jambo baya. Mfano jirani ambaye anamuona house girl wako akiingiza wanaume kipindi umeenda kazini na mkeo, huku nyuma watoto wako wadogo wanashuhudia mambo ya ufuska yanayofanywa na beki 3. Hauonj umbea wake utaokoa mali zako kutokana na wizi wa kuaminiwa na kuokoa watoto wako wasiharibiwe tabia na beki tatu. So umbea una faida
Ila mnafiki sio mtu mzuri sababu analengo la kufitini kama sio kuchonganisha au kurubuni. Anajificha katika sura ambayo si yake ili akupumbaze udhurike.
Imagine una mkeo ana marafiki wanatoka nae wanasema wanakwenda kanisani au vikao vya wanawake kumbe wanamsindikiza kwa wanaume ile hali wakijua mna ndoa halali ya kuheshimishwa. Halafu wanajua mwenzao anaharibu ila wanaona wamchochee aharibu ili awe nungayembe kama wao na wewe ni mtu mzuri kwao ila wanakuzeveza uingie mkenge.