Hivi kati ya Ringo na Tin white au Tin white na Mkojani

mimi nawapenda wote, inaonekana tin ana uwezo mzuri wa kufanya combination na waigizaji wengi na mambo yakaenda vizuri

ukimwangalia tin na ringo kwenye utani utacheka ufe

ukimwangalia tin na mkojani kwenye wajumbe kama wajumbe utacheka ulie machozi yote

ukimwangalia tin na masantula aaah weee huyu tin ni kiboko asee.
 
Hao jamaa nilikuwa na-ignore mwanzoni, badae nikajikuta navutiwa nao.

Mtu anawaponda watu wa vichekesho ila anasikiliza bongo flava.
kusema kwamba sijawahi kuvutiwa na kazi zao ni kujiona wa kishua!!!naonaga ni too childish ndivyo hivyo,sijakuzuia wewe kucheka mpaka meno yako yote 32 kuwa nje!!!kupanga ni kuchagua
 
Sijuagi hata huwa wanaigizaga nini hawa!!yaani nikiona watu wanacheka maigizo ya hawa jamaa huwa nashangaaga sana!!nikiwa kwenye basi ni heri niweke Earphone masikioni nisikilize hata mapambio
Na kuna watu wanashangaa enjoyments zako vile vile. Kwenye hii dunia just keep in mind one thing, huwezi ukavutiwa na kila kitu.
 
Sijuagi hata huwa wanaigizaga nini hawa!!yaani nikiona watu wanacheka maigizo ya hawa jamaa huwa nashangaaga sana!!nikiwa kwenye basi ni heri niweke Earphone masikioni nisikilize hata mapambio
nimeamini tatizo la afya ya akili lipo
 
Sijuagi hata huwa wanaigizaga nini hawa!!yaani nikiona watu wanacheka maigizo ya hawa jamaa huwa nashangaaga sana!!nikiwa kwenye basi ni heri niweke Earphone masikioni nisikilize hata mapambio
Hata Mimi sjuagi hata wanachochekesha , naonaga kama maigizo Fulani yasiyoeleweka , Kwa mtu ambaye ana exposure kidog unaweza kuwaona hawa ni wehu ,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…