Hivi Kati ya Ronaldo De lima na Romario na zaidi?

De Lima kiumbe kingine kile, shida ni anasa na majeruhi.
 
Huyu De Lima aliwahi kusema huwa anapenda kufunga goli baada ya kuwapita mabeki wote pamoja na kipa kwa sababu ndivyo alivyo.

Kuwapita mabeki wote ni kazi ya Messi na Diego. Wengine wakasome kwanza
 
Ni ngumu kidogo kama umewahi kuwatizama wote katika vipindi vyao.
Wengi watasema Ronaldo de Lima kwa kuwa kizazi hiki kilimtazama na kumuona.
Wengi watasema Ronaldo kwa kuwa alicheza zama ambazo fursa ya kuangalia mpira ilikuwa kwa watu wengi zaidi.
Nimemuona Romario wakati wa Fainali ya kombe la Dunia mwaka 1994 USA.
Nimemuona Romario wakati wa kombe la America kusini miaka ya 1992 -1997.
Romario ni mchezaji namba tano katika orodha ya wachezaji wa karne huku Ronaldo akishika namba saba katika orodha hiyo.
Nimemuona Ronaldo akiwa na Brazil na kuiongoza kutwaa kombe la dunia. Nilimuona Ronaldo akitwaa tunzo kadhaa barani Ulaya na Duniani.
Ni ngumu kuwalinganisha miamba hawa lakini kwangu Romario De Souza anazidi kidogo.
shukrani kwa kuleta hili
 
Romario alitamba sana kwao Brazil na kombe la dunia Kule Marekani akiwa na Bebeto ila ki ukweli na bila ubishi bila mizengwe Ronaldo de Lima ni habari nyingine kwa upande wa namba 9. Dunia itachukua muda kupata kiumbe namna 9 kama Ronaldo de Lima. Mpinzani wa Romalio alikua Edmundo walishindana sana uko Brazil. Romario amecheza mda mfupi Ulaya hasa pale Barca.
 
Hhmmmm... Swali gumu sana hili hawa miamba ni hatari wanashabihiana kwa kiasi kubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…