Hivi Katiba Mpya ni takwa binafsi la kiongozi au ni takwa la watu anaowaongoza?

Hivi Katiba Mpya ni takwa binafsi la kiongozi au ni takwa la watu anaowaongoza?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Mnapokuwa na kiongozi ambae anafikiri priorities zake ndio muhimu kuliko priorities za watu anawaongoza, basi jamii husika ijue imekula hasara kuwa na kiongozi wa aina hiyo.

Watu wengine hawafai kuwa viongozi maana hawajui nini maana ya kuongoza.Kama husikilizi sauti/mawazo ya walio wengi, tambua teyari umepoteza sifa za kuwa kiongozi na huenda umekuwa kiongozi kwa bahati mbaya tu.

Cheza na "kula" lakini kamwe usicheze na "kura" yako na pambana na yoyote anaechezea kura yako kwani inaweza kukugharimu maisha yako yote.

2020 ni mwaka wa kusahihisha makosa. Mnaoksea mnatuponza wengi.
 
Kwa bahati mbaya hapa nchi kwetu, Katiba mpya inaonekana ni takwa la mtu mmoja, mpaka apende yeye. Tawala za kiafrika ni hovyo sana. Binadamu wanajivika u-Mungu.

Yaani Rais wetu mtu mwema kwake ni yule anayemsifia na kumtukuza tu, walio kinyume na mawazo yake wote amewaweka katika kundi la maadui wa Taifa.

Ni hatari sana.
 
Tumerudishwa enzi za gereza la fikra yakinifu
tapatalk_1540809541224.jpeg
 
Rais anatekeleza ilani ya chama cha mapinduzi!
 
Kwanza kosa tulianza kuitafuta katiba bila kuwa na Elimu ya uraia na faida ya katiba kwa wananchi, so inaonekana ni wanaharakati,wapinzani etc,na wananchi wanabaki dilema hawajui wafuate lipi
 
2020 ni mwa wa Kusahihisha makosa kivipi mkuu?
 
Yaani leo hii akubali kuweka sheria zitakazomnyima "nguvu" ya kutawala? Hebu mwacheni huyo "Mfalme Juha" amalize muda wake aondoke zake "Chato" huyo atakayekuja ataendeleza ilipoishia awamu ya nne.
 
Mimi nimeshasitaafu kupanga foleni eti kisa kupiga kura
 
Msilie sana machozi yenu yamefika mbinguni Mungu wetu hajalala usingizi, ukombozi unakuja.
 
Mnapokuwa na kiongozi ambae anafikiri priorities zake ndio muhimu kuliko priorities za watu anawaongoza, basi jamii husika ijue imekula hasara kuwa na kiongozi wa aina hiyo.

Watu wengine hawafai kuwa viongozi maana hawajui nini maana ya kuongoza.Kama husikilizi sauti/mawazo ya walio wengi, tambua teyari umepoteza sifa za kuwa kiongozi na huenda umekuwa kiongozi kwa bahati mbaya tu.HostGator DreamHost Bluehost

Back
Top Bottom