Ili kueteleza Maendeleo ya Nchi yetu na Kupunguza tatizo la Watu kukimbilia Arusha, Dsm, na Mwanza Ni lazima Serikali ikawa na Mipango endelevu ya ku-balance Shughuli za Kilimo na Uendelevu wa Shughuli Nyingine za Kibiashara Kama Viwanda Ambayo Itakuwa Pia ni Kichocheo cha Kuendeleza Miundo Mbinu Mingine Kama Barabara, Umeme, Nyumba Bora na Elimu. Ni meliona tatizo Hili Hususana Katika Mikoa ya Shinyanga, Singida, Tabora, Lindi, na Ruvuma, mfano
Singida, wana Potential Kubwa saana ya Kimaendeleo Lakini Kikwazo Cha Barabara na Umeme Unakwanza Juhudi za Kuibadili Singida, Au ndio Tuna Subiri Jumuiya ya Afrika Mashariki Ichoche hayo Maendeleo? na Hata Mkoa Wa Ruvuma Hali Ni Hiyo Hiyo Mpaka Mbinga. Pale Singida kuna Alizeti, Kuna Pamba , Vitungu , Kuku wa Kienyeji, Mbuzi nk
JK afungua Kiwanda Cha Nguo USA River Arusha
Wawekezaji nchini wametakiwa kuwekeza katika viwanda vya kutengeneza nyuzi, nguo na kushona mavazi kwani kwa kufanya hivyo si tu wataongeza ajira na mapato ya nchi, bali pia watawahakikishia wakulima wa zao la pamba masoko ya uhakika na bei nzuri ya zao hilo.
Rai hiyo ilitolewa juzi na Rais Jakaya Kikwete wakati akizungumza na wananchi pamoja na wafanyakazi wa Kiwanda cha kutengeneza nyuzi cha Jambo Spinning Mill kilichopo Usa River mkoani Arusha mara baada ya kufungua kiwanda hicho.
Rais Kikwete alisema kinachotakiwa hivi sasa ni kuongeza uzalishaji wa zao la pamba kwani kwa wastani, wakulima nchini wanazalisha kilo 200, 250 hadi kilo 300 wakati wakulima wa nchi za nje wanazalisha kilo 800 mpaka zaidi ya kilo 1,000 kwa hekta.
Sisi tunao uwezo wa kuzalisha pamba kwa wingi zaidi ya tunayoizalisha hivi sasa mara mbili hadi tatu kama tutaamua kwani bado hatujaanza kazi ya kuzalisha pamba hadi ikafika mahali tukajidai na hii ni moja ya shabaha kubwa ya serikali katika mkakati wa kusukuma kilimo kwa kasi kubwa zaidi ujulikanao kama Kilimo Kwanza, alisema Rais Kikwete. Rais Kikwete alisema serikali inatambua umuhimu wa sekta binafsi na wawekezaji nchini hivyo basi ina jukumu la kuweka mazingira mazuri ili wawekezaji wengi zaidi waje kuwekeza.
Hivi sasa serikali inaondoa vikwazo vya kuzuia uwekezaji hapa nchini inachofanya ni kuharakisha utoaji wa leseni, kuondoa urasimu katika masuala ya ulipaji wa kodi, kuwezesha viongozi na watendaji wa serikali kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati mwafaka na kuwezesha shughuli za uwekezaji kufanyika katika uwazi na kumalizika katika kituo kimoja, alisema.
Aidha, Rais Kikwete pia aliwataka wamiliki wa kiwanda hicho kujitahidi kuangalia maslahi ya wafanyakazi wao kwani kama watawaenzi na wao watafanya kazi kwa bidii na uaminifu, jambo litakalowezesha kiwanda kudumu na kutoa huduma inayotakiwa kwa wananchi.
Akisoma taarifa ya kiwanda hicho, Mkurugenzi Mtendaji wake, Salum Hamis Salum alisema nyuzi zinazotengenezwa katika kiwanda hicho, zinatokana na pamba ya nchini inayochambuliwa na kiwanda tanzu na hicho cha Jambo Ginnery kilichopo mkoani Shinyanga. Salum alisema matarajio ya kiwanda hicho ni kufikia uwezo wa kufuma nguo za kisasa, kwa matumizi ya ndani na nje ya nchi huku wakiwa na lengo la kuingia katika soko la AGOA.
"Changamoto zinazotukabili ni kuyumba kwa uchumi wa dunia ambako kwa kiasi kikubwa kumeathiri sana soko la nyuzi na gharama kubwa za uendeshaji wa kiwanda ikiwa ni pamoja na kupanda kwa gharama za umeme, alisema Salum. Mwaka 2004, Watanzania wanaomiliki kiwanda hicho walianza uwekezaji wa zaidi ya dola za Marekani milioni 50 katika ujenzi. Matarajio yao ni kukipanua zaidi kwa kuongeza uwekezaji hadi kufikia dola za Marekani milioni 200. Kwa sasa kina wafanyakazi 220 na matarajio ni kuwa na wafanyakazi 1,000