Kama kuna kiumbe anaweza kunielewesha nitashukuru, kwa maana nimekuwa sielewi kinachoendelea nchini Kenya, kulikuwa na uchaguzi wa Uraisi, wabunge ukaisha washindi wakapatikana, akiwemo Raisi mpya Bw.Uhuru Kenyata sasa ni kwa nini kila siku mara maandamano hapa, mara fujo pale mara hawa hawamtaki Raisi Uhuru, mara sijui wanataka kumtoa kwa maandamano, sasa hii yote ni ya nini?
Kama kulikuwa na Uchaguzi na Mshindi akapatikana kwa nini wote msiungane na kushirikiana naye mpaka Uchaguzi mwingine utakapofika? Tatizo ni nini? Na kama hawamkubali Mshindi ni kwa nini hata wanafanya Uchaguzi na kupoteza fedha nyingi za walipa kodi?